Fanya lolote kwa kusudi jema , utafanikiwa

Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu, bali jibu la ulimi hutoka kwa BWANA. Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe, bali makusudi hupimwa na BWANA. Mkabidhi BWANA lo lote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa.

Mithali 16:1-3

Ukiwa na Imani , Utafanikiwa

Matayo 5:42-46

Imani Kidogo Huleta Mabadiliko
Imani Kidogo Huleta Mabadiliko

‘‘Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Ninawaambia kweli, mkiwa na imani kama punje ndogo ya haradali, mtauambia mlima huu, ‘Ondoka hapa uende pale’ nao utaondoka. Wala hakutakuwa na jambo lisilowezekana kwenu.

Tuseme nini basi kuhusu haya? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani awezaye kuwa kinyume chetu?

Omba Mungu Anasikia na Atajibu

Isaya 38: 1-6

Katika siku hizo Hezekia akaugua naye akawa karibu na kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akamwendea na kumwambia, “Hili ndilo asemalo BWANA: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”

Hezekia akageuza uso wake kuelekea ukutani na kumwomba BWANA, “Ee BWANA, kumbuka, jinsi nilivyotembea mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wote nami nimefanya lile lililo jema machoni pako.” Naye Hezekia akalia sana sana.

Ndipo neno la BWANA likamjia Isaya: “Nenda ukamwambie Hezekia, ‘Hili ndilo asemalo BWANA, Mungu wa baba yako Daudi: Nimesikia maombi yako na nimeona machozi yako, nitaiongeza miaka kumi na mitano katika maisha yako. Nami nitakuokoa wewe pamoja na mji huu kutoka katika mkono wa mfalme wa Ashuru. Nitaulinda mji huu.

Upendo Kwa Adui

‘‘Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Mpende jirani yako na umchukie adui yako.’ Lakini mimi ninawaambia, Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa ninyi, ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana Yeye huwaangazia jua lake watu waovu na watu wema, naye huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. Kama mkiwapenda wale wanaowapenda tu, mtapata thawabu gani? Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo?

Matayo 5:43-46