Thawabu Ya Kumtii BWANA

Zaburi ya 128


Heri ni wale wote wamchao BWANA,

waendao katika njia zake.

Utakula matunda ya kazi yako,

baraka na mafanikio vitakuwa vyako.

Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao

katika nyumba yako,

wana wako watakuwa kama machipukizi ya

mizeituni kuizunguka meza yako.

Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu

amchaye BWANA .

BWANA na akubariki kutoka Sayuni

siku zote za maisha yako,

na uone mafanikio ya Yerusalemu,

nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa

watoto wako.

Amani iwe juu ya Israeli.

Kwa maana Yeye ni Mungu aliye hai, Huponya na Kuokoa

Tafakali ya Leo

Kila mmoja wetu kama ilvyokuwa kwa Daniel anaweza akawa katika tundu la simba, tundu lako laweza kuwa ungonjwa ulionao, haki uliyodhulumiwa kazini, matatizo katika ndoa yako, nk. Lakini kumbuka, kama vile Mungu alivyomtuma malaika akafunga vinywa vya simba wasimdhuru Daniel , ndugu yangu kuwa na faraja kwa kuwa Mungu wetu ni Mungu aliye hai , huponya na kuokoa,  anaona masumbuko yako, na mwombe naye atatuma malaika wake aje akuokoe kutoka katika tundu hila la masumbuko yako.

Dainel 6:16, 18, 21 ,25-27

Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli wakamtupa ndani ya tundu la simba. Mfalme akamwambia Danieli, ‘‘Mungu wako unayemtumikia daima na akuokoe!’’

Kisha mfalme akarudi kwenye jumba lake la kifalme na usiku kucha hakula chakula wala kutumia viburudisho alivyoletewa. Wala hakuweza kulala.

Danieli akajibu, “Ee mfalme, uishi milele! Mungu wangu alimtuma malaika wake, naye akafunga vinywa vya hawa simba. Hawajanidhuru, kwa sababu nilionekana sina hatia mbele zake. Wala kamwe sijafanya jambo lo lote baya mbele yako, Ee mfalme.’’

Kisha mfalme Dario akawaandikia kabila zote za watu, mataifa na watu wa kila lugha katika nchi yote:

“Ninyi na mstawi sana!  “Natoa amri hii kwamba katika kila sehemu ya ufalme wangu lazima watu wamwogope na kumheshimu Mungu wa Danieli.

Kwa maana Yeye ni Mungu aliye hai naye hudumu milele,

ufalme wake hautaangamizwa, nao utawala wake kamwe hauna mwisho.

Huponya na kuokoa:

hufanya ishara na maajabu mbinguni na duniani. Amemponya Danieli kutoka katika nguvu za simba.’’

Roho wa Mungu Hutuongoza Kuyashinda Majaribu ya Ibilisi

Tafakali

Shetani au ibilisi hutumia maandiko ili kutuingiza dhambini, ni muhimu kila unaposikia andiko kumuomba Roho wa Mungu akuangazie kujua kama ni tamko la Mungu kweli ama ni hila za Ibilisi. Majaribu yapo tumwombe Mungu atusaidia kuyakabili.

Luka 4:1-13

Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani akaongozwa na Roho Mtakatifu hadi jangwani, mahali ambako kwa siku arobaini alikuwa akijaribiwa na Ibilisi. Kwa siku zote hizo hakula cho chote, hivyo baada ya muda huo akaona njaa.

Ibilisi akamwambia, “Ikiwa Wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate.” Yesu akajibu akamwambia, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, bali kwa kila neno la Mungu.’ ”

Ibilisi akampeleka hadi juu ya mlima mrefu akamwonyesha milki zote za dunia kwa mara moja. Akamwambia, “Nitakupa mamlaka juu ya milki hizi na fahari zake zote, kwa maana zimekabidhiwa mikononi mwangu nami ninaweza kumpa ye yote ninayetaka. Hivyo ikiwa utanisujudia na kuniabudu, vyote vitakuwa vyako.”

Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mwabudu Bwana Mungu wako na umtumikie Yeye peke yake.’ ”

Kisha Ibilisi akampeleka mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya mnara mrefu mwembamba wa hekalu, akamwambia, “Kama Wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini kutoka hapa, kwa maana imeandikwa: “ ‘Atakuagizia malaika zake wakulinde, nao watakuchukua mikononi mwao usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’ ”

Yesu akamjibu, “Imesemwa, ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’ ”

Ibilisi alipomaliza kila jaribu, akamwacha Yesu mpaka wakati mwingine ufaao.

Sikiliza Mafundisho ya Wazazi na Wala Usifuatane na Wenye Dhambi

Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako,wala usiyaache mafundisho ya mama yako.  Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako, na mkufu shingoni mwako.


Mwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi, usikubaliane nao.


Kama wakisema, “Twende tufuatane, tukamvizie mtu na kumwaga damu, njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia, tuwameze wakiwa hai kama kaburi, wakiwa wazima wazima kama wale wanaotumbukia shimoni, tutapata aina zote za vitu vya thamani na kujaza nyumba zetu kwa nyara, njoo ushirikiane nasi, vitu vyote tutakavyopata tutagawana.’’


Mwanangu, usiandamane nao, usiweke mguu wako katika njia zao, kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi, ni wepesi kumwaga damu.

MITHALI 1:8-16

Mungu Huwabariki na Kuwapa Thawabu Wanaomkubali Mwana Wa Mungu – Yesu

Akawatazama wanafunzi wake akasema:

Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, kwa sababu Ufalme wa Mbingini ni wenu.

Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashibishwa.

Mmebarikiwa ninyi mnaolia sasa, kwa sababu mtacheka.

Mmebarikiwa ninyi watu watakapowachukia, watakapowatenga na kuwatukana na kulikataa jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.

Furahini na kurukaruka kwa shangwe kwa sababu thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo baba zao walivyowatenda manabii.

LUKA 6: 20-23

Karibu sana katika NenoLaFaraja. NeloLaFaraja ni maalumu kwetu sote, linakuja kwa ajili yakupeana maneno mazuri ya Mungu, kuna blog za nyingi sana hiini mojawapo ambayo itakupa neno ya tumaini na la kufariji katika maisha yetu ya kimwili na kiroho, ndiyo maana namshukuru Mungu kuanza kwa NenoLaFaraja.

Karibu sana na jisikie huru kutoa maoni yako ya kujenga kiroho na kimwili wakati wowote, maoni yote yataonekana, tuma kwa e-mail nenolafaraja@gmail.com.

NenoLaFaraja itakuwa upadated kila baada ya saa 24.

Tafadhali wajulishe na wengine kuhusu NenoLaFaraja.

Ubarikiwe sana na Karinu sana.

NenoLaFaraja (neno)

Uniiite Siku Ya Taabu Nami Nitakuokoa Nawe Utanitukuza

Mwenye Nguvu, Mungu, BWANA, asema na kuiita dunia, tangu mawio ya jua hadi mahali pake liendapo kutua.

Kutoka Sayuni, penye uzuri mkamilifu, Mungu anaangaza. Mungu wetu anakuja na hatakaa kimya, moto uteketezao unamtangulia, akiwa amezungukwa na tufani kali. Anaziita mbingu zilizo juu na nchi, ili aweze kuwahukumu watu wake:

Kwa maana kila mnyama wa msituni ni wangu, nayo makundi ya mifugo juu ya vilima elfu. Ninamjua kila ndege mlimani, nao viumbe wa kondeni ni wangu. Kama ningekuwa na njaa nisingewaambia ninyi, kwa maana ulimwengu ni wangu, pamoja na vyote vilivyomo ndani yake.

Toa sadaka za shukrani kwa Mungu, timiza nadhiri zako kwake Yeye Aliye Juu Sana na uniiite siku ya taabu nami nitakuokoa nawe utanitukuza

ZABURI 50:1-4,10-12,14-15