Pendaneni

‘Amri mpya nawapa: Mpendane kama Mimi nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane. Kama mkipendana ninyi kwa ninyi, kwa njia hii, watu wote watajua kuwa ninyi ni wanafunzi Wangu’’

Yohana 13:34-35

Mwite Bwana katika shida yako , Atasikia

‘‘Katika shida yangu nalimwita BWANA,

naye akanijibu.

Kutoka kina cha kaburi niliomba msaada,

nawe ukasikiliza kilio changu.

Ulinitupa kwenye kilindi,

ndani kabisa ya moyo wa bahari,

mikondo ya maji ilinizunguka,

mawimbi yako yote na viwimbi vilipita juu

yangu.

Nikasema, ‘Nimefukuziwa mbali na uso wako,

hata hivyo nitatazama tena kuelekea hekalu

lako takatifu.

5Maji yaliyonimeza yalinitisha,

kilindi kilinizunguka,

mwania ulijisokota kichwani pangu.

Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho

za milima,

makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata

milele.

Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni,

Ee BWANA Mungu wangu.

Yona 2:2-6

Yapokee Mafundisho ya Mungu


Uyapokee mafundisho toka kinywani mwake

na maneno yake uyaweke moyoni mwako.

Kama ukimrudia Mungu Mwenye Nguvu,

utarudishwa upya:

Kama ukiuondoa uovu uwe mbali na hema

Lako,

kama dhahabu yako ukiihesabu kama

mavumbi,

dhahabu yako ya Ofiri kama miamba ya

mabondeni,

ndipo Mungu Mwenye Nguvu atakuwa

dhahabu yako

naye atakuwa fedha yako iliyo bora.


Ayubu 22:22-25

Mlilie Mungu Naye Atakusikiliza

Ee BWANA, usikie sala yangu,

kilio changu cha kuomba

msaada kikufikie.

Usinifiche uso wako

ninapokuwa katika shida.

Unitegee sikio lako,

ninapoita, unijibu kwa upesi.

Mataifa wataogopa jina la BWANA, wafalme wote wa dunia

watauheshimu utukufu wako.

Kwa maana BWANA ataijenga tena Sayuni

na kutokea katika utukufu wake.

Ataitikia maombi ya mtu mkiwa,

wala hatadharau hoja yao

Hili na liandikwe kwa ajili ya kizazi kijacho,

ili taifa litakaloumbwa baadaye waweze

kumsifu BWANA :

“ BWANA alitazama chini kutoka

patakatifu pake palipo juu,

kutoka mbinguni alitazama dunia,

kusikiliza vilio vya uchungu vya wafungwa

na kuwaweka huru wale waliohukumiwa

kufa.’’

ZABURI 102:1-2, 15-20

Mungu Mlinzi Wetu

Yeye akaaye mahali pa salama pake

Yeye Aliye Juu sana,

atadumu katika uvuli wake Mungu

Mwenye Nguvu zote.

Nitasema kuhusu BWANA,

“’Yeye ndiye kimbilio langu

na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye

ninamtumaini.’’

Hakika yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji

na maradhi ya kuambukiza ya kufisha.

Atakufunika kwa manyoya yake,

chini ya mbawa zake utapata kimbilio,

uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako.

Hutaogopa vitisho vya usiku,

wala mshale urukao mchana,

wala maradhi ya kuambukiza yanayonyemelea

gizani, wala tauni iharibuyo adhuhuri.

Zaburi 93:1-6

===

Sala Yangu Leo

Nitakusifu wewe bwana Mungu wangu

kwa moyo wangu wote

na kulitukuza jina lako milele.

Amina

Hakuna aliye Mkuu kama Mungu

Ee BWANA,

mbingu zinayasifu maajabu yako,

uaminifu wako pia,

katika kusanyiko la watakatifu.

Kwa kuwa ni nani katika mbingu juu anayeweza

kulinganishwa na BWANA ?

Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni

aliye kama BWANA ?

Katika kusanyiko la watakatifu Mungu

huogopwa sana,

anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka.

Ee BWANA Mwenye Nguvu, ni

nani aliye kama Wewe?

Ee BWANA, Wewe ni mwenye nguvu,

na uaminifu wako unakuzunguka.

Zaburi 88:5-8

Sala yangu Leo

Ee Mungu uniokoe

maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu,

ninazama katika matope mengi

nategemea nguvu zako,

Amina.

Umuhimu Wa Kuwa Na Imani

Basi, kujivuna kuko wapi? Kumewekwa mbali. Kwa sheria gani? Je, ni kwa ile ya matendo? La hasha, bali kwa ile sheria ya imani. Kwa maana twaona kwamba mwanadamu huhesabiwa haki kwa njia ya imani wala si kwa matendo ya sheria. Je, Mungu ni Mungu wa Wayahudi peke yao? Je, Yeye si Mungu wa watu Mataifa pia? Naam, Yeye ni Mungu wa watu Mataifa pia.

Warumi 3:27-29

Sala Yangu Leo

Mungu uisikie sauti yangu

katika malalamiko yangu

unilinde uhai wangu

na hofu ya adui zangu

Mimi Nimewachagua Kutoka Katika Ulimwengu

‘‘Kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni kwamba ulinichukia Mimi kabla yenu. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungeliwapenda kama vile unavyowapenda walio wake. Kwa sababu ninyi si wa ulimwengu, lakini Mimi nimewachagua kutoka katika ulimwengu, hii ndiyo sababu ulimwengu unawachukia. ‘Kumbukeni lile neno nililowaambia, ‘Hakuna mtumishi aliye mkuu kuliko bwana wake.’ Kama wamenitesa Mimi, nanyi pia watawatesa, kama wamelishika neno langu, watalishika na neno lenu pia.

Yohana 15-19-20

Sala Yangu Leo…

Ee Mungu wangu nitakutafuta mapema asubuhi

maana nafsi yangu inakuonea kiu

na kukutegemea wewe peke yako.

Amina

Tayari Kwa Siku Ya Bwana

Basi, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira hatuna haja ya kuwaandikia, kwa kuwa mnajua vema kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwivi ajapo usiku. Wakati watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafla kama vile utungu umjiavyo mwanamke mwenye mimba wala hawatatoroka.

1 Wathesolanike 5:1-3

Sala yangu Leo…

Nafsi Yangu Umgoje Mungu

Peke Yake Kwa Kimya,

Tumaini Langu Kwake Yeye tu

Ndiye Mwamba Wangu,

Amina.