Sifa Za BWANA

Msifuni BWANA, mataifa yote,

mtukuzeni yeye, enyi mataifa

yote.

Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu,

uaminifu wa BWANA unadumu milele.

Msifuni BWANA

Zaburi 117:1-2


Mwenye Hekima Husikiwa

Maneno ya utulivu ya mwenye hekima

husikiwa kuliko makelele ya mtawala wa

wapumbavu.

Hekima ni bora kuliko silaha za vita,

lakini mwenye dhambi mmoja huharibu

mema mengi.

MHUBIRI 9:17-18

Tudumishe Umoja Katika Familia Kama Umoja Katika Mwili Wa Kristo

Basi, mimi niliye mfungwa wa Bwana, nawasihi mwenende kama inavyostahili wito wenu mlioitiwa. Iweni wanyenyekevu kabisa na wapole, mkiwa wavumilivu, mkichukuliana kwa upendo. Jitahidini kudumisha umoja wa Roho katika kifungo cha amani. Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja. Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote na ndani ya yote.

WAEFESO4:1-6


Uwe Hodari Katika Neema Iliyo Ndani Ya Kristo Yesu, Nawe Utabarikiwa

Vumilia taabu pamoja nasi kama askari mwema wa Kristo Yesu. Hakuna askari ye yote ambaye akiwa vitani hujishughulisha na mambo ya kawaida ya maisha haya kwa sababu nia yake ni kumpendeza yule aliyemwandika awe askari. Vivyo hivyo, yeye ashindanaye katika michezo hawezi kupewa tuzo ya ushindi asiposhindana kulingana na kanuni za mashindano.Mkulima mwenye bidii ya kazi ndiye anayestahili kuwa wa kwanza kupata fungu la mavuno.

2 Timotheo 2:3-6


Tumaini Huleta Saburi

Si hivyo tu, bali twafurahi pia katika mateso, kwa sababu tunajua kuwa mateso huleta saburi, nayo saburi huleta uthabiti wa moyo na uthabiti wa moyo huleta tumaini, wala tumaini halitukatishi tamaa, kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo Lake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ametupatia.

Warumi 5:3-5

Mtolee Mungu kwa Moyo

Yesu alipoinua macho yake, aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la hazina ya hekalu. Akamwona pia mwanamke mmoja mjane maskini, akiweka humo sarafu mbili za shaba. Yesu akasema, “Amin, amin nawaambia, huyu mjane maskini ameweka humo sadaka kubwa zaidi kuliko wengine wote. Hawa watu wengine wote wametoa sadaka kwa Mungu kutokana na wingi wa mali zao, lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake vyote alivyokuwa navyo kwa ajili ya maisha yake.”

Luka 21:1-4

Yesu Ndiye Njia Ya Kwenda Kwa Baba

Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu, mnamwamini Mungu, niaminini na Mimi pia. Nyumbani mwa Baba Yangu kuna makao mengi. Kama sivyo, ningeliwaambia. Nakwenda kuwaandalia makao. Nami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. Ninyi mnajua njia ya kufika ninakokwenda.’’

Yohana 14: 1-4