Furahi Kila Siku, Kwa Kuwa Furaha Ya BWANA Ni Nguvu Zenu.

Nehemia akasema, “Nendeni mkafurahie chakula kizuri na vinywaji vitamu, na mpeleke sehemu kwa wale ambao hawana cho chote cha kula. Siku hii ni takatifu kwa BWANA. Msihuzunike, kwa kuwa furaha ya BWANA ni nguvu zenu.

Nehemia 8:10

Go and enjoy choice food and sweet drinks
Go and enjoy choice food and sweet drinks

Mche Mungu na Ridhika na Kidogo Alichokujalia

Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha BWANA,

kuliko mali nyingi pamoja na ghasia.

Afadhali chakula cha mboga mahali palipo na upendo

kuliko nyama ya ndama iliyonona pamoja na chuki,

Mithali 15:16-17

Better a little with the fear of the LORD
Better a meal of vegetables where there is love than a fattened calf with hatred.

Mungu Mlinzi Wa Watu Wake

Kama BWANA asingalikuwa upande wetu,

wakati watu walipotushambulia,

wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu,

wangalitumeza tungali hai,

BWANA asifiwe,

yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe

kwa meno yao.

Msaada wetu ni katika jina la BWANA,

Muumba wa mbingu na dunia

Zaburi 124:2-3,6,8

Our help is in the name of the LORD, the Maker of heaven and earth.
Our help is in the name of the LORD, the Maker of heaven and earth.


Kwa Neno Tu, Yesu Atataua Shida Zako Zote, Amini

Hivyo Yesu akaongozana nao, lakini alipokuwa hayuko mbali na nyumbani, yule jemadari akatuma rafiki zake kumwambia Yesu, “Bwana, usijisumbue kwani mimi sistahili Wewe kuingia chini ya dari yangu. Ndiyo maana sikujiona ninastahili hata kuja kwako. Lakini sema neno tu, naye mtumishi wangu atapona.

Yesu aliposikia maneno haya alimshangaa sana, akaugeukia ule umati wa watu uliokuwa unamfuata, akawaambia, “Sijaona imani kubwa namna hii hata katika Israeli.” Nao wale watu waliokuwa wametumwa kwa Yesu waliporudi nyumbani walimkuta yule mtumishi amepona.

Luka 7:6-7, 9-10