Are your dreams fake, dead or alive?

I recently bought a plant for my living room. I knew it was real, but some of my friends thought it was fake. We forgot to water it for a month and it was still green. One friend said, “See…it is fake.” They actually thought it was funny that I believed it was real. I began to doubt what I knew was true.

After an extended overseas trip, I came home to find this plant was drooping down limp and its color was bright yellow. I couldn’t believe my eyes. It was real! Today what dreams or hopes do you think are fake? You might even become so convinced you stop watering those aspirations altogether. Yet I want to encourage you: with God nothing is impossible. Maybe today, if you nourish your mind and heart from the living waters of His Word, the dreams God has given you will not only survive, but thrive.

In Him, Through Him, For Him,
Credit: Nick Vujicic

With God nothing is impossible.

Unataka Nini Kutoka Kwa Yesu, Mwambie Atakupatia

Yesu aliposhuka kutoka mlimani, makutano makubwa ya watu yakamfuata. Mtu mmoja mwenye ukoma akaja na kupiga magoti mbele yake akasema, “Bwana, kama ukitaka, unaweza kunitakasa.’

Yesu akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka, takasika!’’

Matayo  8:1-3

Tafakari.

Yesu yupo tayari kukufanyia kitu chochote unachotaka, kama tu ukimwendea ukamweleza kwa imani.

Lord, if you are willing, you can make me clean
"I am willing," he said. "Be clean!"

Mungu Anakuthamini Sana Usiwe na Wasiwasi

‘‘Kwa hiyo nawaambia, msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini, au kuhusu miili yenu, mtavaa nini. Je, maisha si zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, wao hawapandi wala hawavuni au kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Je, ninyi si wa thamani zaidi kuliko hao ndege?

Kwa hiyo msiwe na wasiwasi, mkisema, ‘Tutakula nini?’ Au ‘Tutakunywa nini?’ Au ‘Tutavaa nini?’ Kwa maana watu wasiomjua Mungu ndio wanaoshindania hayo, lakini Baba yenu wa mbinguni anafahamu kwamba mnahitaji hayo yote. Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake na haya yote mtaongezewa.

Matayo 6:25-26, 31-33

Usigope wala Kufadhaika, Mungu hatakuacha kwa lolote

Iweni imara na moyo wa ushujaa. Msiogope wala msifadhaike kwa sababu yao, kwa kuwa BWANA Mungu wenu anakwenda pamoja nanyi, kamwe hatawaacha wala hatawatupa ninyi.’

Kumbukumbu la Torati 31:6

Tafakari

Kama una matatizo au una wasiwasi na kitu chochcote leo, basi ndugu yangu mshukuru Mungu kwani hatakuacha pekee, Mungu ana mipango yake katika kila jambo linalotokea, usiogope, kuwa na imani na endelea kumuomba kila wakati ukijua fika kuwa Yupo mapoja nawe.

Tumikianeni kwa upendo

Ndugu zangu, ninyi mliitwa ili mwe huru, hivyo msitumie uhuru wenu kama fursa ya kufuata tamaa za mwili, bali tumikianeni ninyi kwa ninyi kwa upendo. Kwa maana sheria yote hukamilika katika amri moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” Kama mkiumana na kutafunana, angalieni, msije mkaangamizana.

But do not use your freedom to indulge the sinful nature; rather, serve one another in love
But do not use your freedom to indulge the sinful nature; rather, serve one another in love

Wagalatia 5:13-15

Mungu ana Mipango ya Kukufanikisha , Mtafute Kwa Moyo na Mweleze Mipango Yako Atakusikiliza

Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,’’ asema BWANA. “Ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo. Kisha mtaniita na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza. Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.

Yeremia 29:11-13

Zaidi Ndani ya Yeremia 29:11-13

Sala Yangu Leo

Sikiliza kilio changu ili unisaidie,

Mfalme wangu na Mungu wangu,

kwa maana kwako ninaomba.

Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee BWANA,

asubuhi naleta haja zangu mbele zako

na kusubiri kwa matumaini.

Niongoze katika haki yako, Ee BWANA,

kwa sababu ya adui zangu,

nyosha njia yako mbele yangu.

Hakuna neno kinywani mwao linaloweza kuaminika,

mioyo yao imejaa maangamizi.

Koo zao ni kaburi lililo wazi,

kwa ndimi zao hunena udanganyifu.

Kwa hakika, Ee BWANA,

unawabariki wenye haki,

unawazunguka kwa wema wako kama ngao.

Zaburi 5:2-3,8-9,12

Hearken unto the voice of my cry, my King, and my God: for unto thee will I pray
My voice shalt thou hear in the morning, O LORD; in the morning will I direct my prayer unto thee, and will look up