UPENDO

Mungu anamipango ya kukufanikisha , Mwamini

Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili
yenu,’’ asema BWANA. “Ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.

Yeremia 29:11

Tafakari

Usikate tamaa Mungu anajua anachokupangia , kwani anapenda ufanikiwe, kwa hiyo katika hali yeyote uliyonayo ona Mungu ana mipango mema kwako

Sala

Eee Mungu baba wa milele, nakushukuru kwa kuwa najua una mipango mema kwangu, nipe nguvu za kufuata mipango yako.

Amina.

http://journeyanswers.com/insignificance?gclid=COHDgeLl7KICFdIB4wodNAN7eg

 

 

Katika Shida na Usiyoyajua Mwite Bwana Mungu atakutikia

Hili ndilo BWANA asemalo, yeye aliyeumba dunia, BWANA aliyeifanya na kuithibitisha, BWANA ndilo jina lake: ‘Niite nami nitakuitika na kukuambia mambo makuu na yasiyochunguzika usiyoyajua.’

Yeremia 33:2-3

Tafakari

Bwana Mungu ni mkuu na husikia wakati wowote umwombapo, jipe moyo na mwite siku zote katika jambo lolote , naye kwa kuwa ana upendo atakusikia na kukutimizia utakayo, shika amri zake.

Sala

Bwana Baba wa Milele, nipe imani ya kukuita kila wakati. Amina