Tupendane sisi kwa sisi.

Hili ndilo neno mlilolisikia tangu mwanzo, kwamba imetupasa tupendane sisi kwa sisi. Msiwe kama Kaini aliyekuwa wa yule mwovu akamwua ndugu yake. Basi kwa nini alimwua? Ni kwa sababu matendo yake Kaini yalikuwa mabaya na ya ndugu yake yalikuwa ya haki. Ndugu zangu, ninyi msistaajabu kama ulimwengu ukiwachukia. Sisi tunajua ya kwamba tumepita kutoka mautini kuingia uzimani, kwa sababu tunawapenda ndugu. Kila asiyempenda ndugu yake akaa mautini.

1 Yohana 3:11-14

Tenda Neno la Mungu , usiwe msikiaji tu, utabarikiwa katika kile unachofanya

Basi iweni watendaji wa Neno wala msiwe wasikiaji tu, huku mkijidanganya nafsi zenu. Kwa maana kama mtu ni msikiaji tu wa Neno wala hatendi kile linachosema, yeye ni kama mtu ajitazamaye uso wake kwenye kioo na baada ya kujiona alivyo, huenda zake na mara husahau jinsi alivyo. Lakini yeye anayeangalia kwa bidii katika sheria kamilifu, ile iletayo uhuru, naye akaendelea kufanya hivyo bila kusahau alichosikia, bali akalitenda, atabarikiwa katika kile anachofanya.

Yakobo 1:22-25

Sala yangu Leo;

Ewe Mungu, Baba wa milele, nipe nguvu za kusoma neneo lako kila mara na kutenda kadili ya neneo hilo. Amina

Amani Moyoni

Perfect Peace

There once was a King who offered a prize to the artist who would paint the best picture of peace. Many artists tried. The King looked at all the pictures, but there were only two he really liked and he had to choose between them.
One picture was of a calm lake. The lake was a perfect mirror for peaceful towering mountains were all around it. Overhead was a blue sky with fluffy white clouds. All who saw this picture thought that it was a perfect picture of peace.
The other picture had mountains too. But these were rugged and bare. Above was an angry sky from which rain fell, in which lightening played. Down the side of the mountain tumbled a foaming waterfall. This did not look peaceful at all.
But when the King looked, he saw behind the waterfall a tiny bush growing in a crack in the rock. In the bush a mother bird had built her nest. There, in the midst of the rush of angry water, sat the mother bird on her nest … perfect peace.
Which picture do you think won the prize?
The King chose the second picture.
Do you know why?
“Because,” explained the King, “peace does not mean to be in a place where there is no noise, trouble, or hard work. Peace means to be in the midst of all those things and still be calm in your heart. That is the real meaning of peace.”

“Nimewaambia mambo haya, ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani Yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana Mimi nimeushinda ulimwengu”

Yohana 16:33

Kile apandacho mtu ndicho atakachovuna

Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna. Apandaye kwa mwili, katika mwili wake, atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa. Kwa hiyo, kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema, hasa wale wa jamaa ya waaminio

Wagalatia 9:7-10