Toa kwa moyo, utabarikiwa

Lakini mjane mmoja maskini akaja na kuweka sarafu mbili ndogo za shaba zenye thamani ya senti mbili.
Yesu akawaita wanafunzi Wake akawaambia, “Amin, amin nawaambia,, huyu mjane maskini ametoa zaidi katika hazina kuliko wengine wote. Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mjane kutokana na umaskini wake, ametoa kila kitu alichokuwa nacho, hata kile alichohitaji ili kuishi.”

Marko 12:42-44

Samehe

Vumilianeni na kusameheana. Mtu akiwa na lalamiko lo lote dhidi ya mwenzake, sameheaneni kama vile Bwana alivyowasamehe ninyi. Zaidi ya maadili haya yote jivikeni upendo, ambao ndio unaofunga kila kitu pamoja katika amani kamilifu.

Wakolosai 3:13-14

Tafakari

Wakolosai 3:13, kama katika Aya nyingine nyingi, Mungu anatoa amri ya kumsamehe kila mmoja. Hii inamaanisha kwamba kama tunataka kusamehewa dhambi zetu lazima kusamehe wale ambao wametukosea au wametenda  dhambi juu yetu, hivyo msamaha ni muhimu sana.

forgive-and-forget
forgive-and-forget
all you need is love
all you need is love

Ni Vizuri Kupendana Kila Mmoja Na Mwingine

Msidaiwe kitu na mtu ye yote, isipokuwa kupendana, kwa maana yeye ampendaye mwenzake, ameitimiza sheria. Kwa kuwa amri hizi zisemazo, “Usizini,” “usiue,” “usiibe,” “usitamani” na amri nyingine zote, zinajumlishwa katika amri hii moja: ‘‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’’ Upendo haumfanyii jirani jambo baya. Kwa hiyo upendo ndio utimilifu wa sheria.

Warumi 13: 8-10

Love One Another

http://www.youtube.com/v/x-eLnMm5Ym8?fs=1&hl=en_US&border=1