Zishike Amri na wafundishe wengine

“Msidhani kwamba nimekuja kuondoa Torati au Manabii, sikuja kuondoa bali kutimiza. Kwa maana,amin, nawaambia, mpaka mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yo yote kutoka kwenye Torati mpaka kila kitu kiwe kimetimia. Kwa hiyo, ye yote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni, lakini ye yote azitendaye na kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu katika Ufalme ya Mbinguni.

Mathew 5: 17-19

Samehe bila kuchoka

Ndipo Petro akamjia Yesu na kumwuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Je, hata mara saba?”
Yesu akamjibu, ‘‘Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.’’

Mathew 18: 21-22

Acha dhambi na uovu, utaishi na Mungu atafurahi

“Lakini mtu mwovu akiacha dhambi zake zote alizozitenda na kushika amri zangu zote na kufanya lililo haki na sawa, hakika ataishi, hatakufa. Hakuna kosa lo lote alilotenda litakalokumbukwa juu yake. Kwa ajili ya mambo ya haki aliyoyatenda, ataishi. Je, mimi ninafurahia kifo cha mtu mwovu? Asema BWANA Mwenyezi. Je, si mimi ninafurahi wanapogeuka kutoka katika njia zao mbaya na kuishi?

Ezekiel 18: 21-23

Zaburi 1: 1-3

Heri mtu yule ambaye haendi
katika shauri la watu waovu,
Wala hafuati njia ya wenye dhambi
au kukaa katika baraza la wenye
mizaha.
2Lakini huifurahia sheria ya BWANA,
nayo huitafakari mchana na usiku.
3Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya
vijito vya maji,
ambao huzaa matunda yake kwa majira na
majani yake hayanyauki.
Kila afanyalo hufanikiwa.

Psalms 1: 1-3

Yoeli 2:12-13

“Hata sasa,’’ asema BWANA,
“Nirudieni kwa mioyo yenu yote,
kwa kufunga, kwa kulia na kuomboleza.’’
Rarueni mioyo yenu
na siyo mavazi yenu.
Mrudieni BWANA, Mungu wenu,
kwa maana yeye ndiye mwenye neema
na mwingi wa huruma,
si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo,
huona huruma hujizuia kupeleka maafa

Joel: 2: 12 -13

Marko 11:24-26

Kwa sababu hiyo nawaambia, yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mmeyapokea nayo yatakuwa yenu. Nanyi kila msimamapo kusali, sameheni, mkiwa na neno na mtu ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi msiposamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.’’

Mark 11: 24-26