Mshukuru Mungu kwa yote

Mshukuruni BWANA, kwa kuwa
Yeye ni mwema,
upendo wake hudumu milele.
2Waliokombolewa wa BWANA na
waseme hivi,
wale aliowaokoa kutoka katika mkono wa adui,
3wale aliowakusanya kutoka nchi mbalimbali,
kutoka mashariki na magharibi,
kutoka kaskazini na kusini

Zaburi 107:1-3

Katika upendo hakuna hofu

Katika upendo hakuna hofu. Lakini upendo ulio kamili huitupa nje hofu, kwa sababu hofu inahusika na adhabu. Kila mwenye hofu hakukamilika katika upendo.
1 Yohana 4: 18