Omba Kila Siku

Mpaka lini Ee BWANA, ? Je

utanisahau, milele?

Utanificha uso wako mpaka lini?

Nitapambana na mawazo yangu mpaka lini

na kila siku kuwa na majonzi moyoni

mwangu?

Adui zangu watanishinda mpaka lini?

Nitazame unijibu, Ee BWANA, wangu.

Uyatie nuru macho yangu ama sivyo

nitalala usingizi wa mauti,

adui yangu atasema, ‘‘nimemshinda,’’

adui zangu watashangilia nitakapoanguka.

Lakini ninategemea upendo wako usiokoma,

moyo wangu unashangilia katika wokovu

wako.

Nitamwimbia BWANA ,

kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.

Zaburi 13

Mungu Anakupenda

Lakini katika mambo haya yote tunashinda, naam na zaidi ya kushinda, kwa Yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua kwa hakika ya kuwa wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuja, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine cho chote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Warumi 8:37-39

Amazing Love (You Are My King)

courtesy: whatchristianswanttoknow.com