Upendo

Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote”

Marko 12:30

Lililo Kuu ni Upendo

Ndugu katika Kristo,

Mungu anapenda tupendane , kwani katika upendo ndipo kila kitu kipo, kama ukimpenda mwenzako, hutamfanyia baya lolole, na hata kama akikukosea basi utakuwa na moyo wa kumweleza hisia zako na kumsamehe,  kwani unampenda, “ basi , sasa na idumu Imani, tumanini, na upendo, haya matatu, na katika hayo lililo kuu ni upendo” 1Wakorinto 13:13.

Na Tuombe:

Mungu mwema, nipe nguvu ya kutimiza amri aliyotuachia Bwana Yesu aliposema  “Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo” Yohana 13:34.

Ninaomba nakushukuru kwa  njia ya Bwana wetu  Yesu Kristu, Amina

The greatest of these is love
The greatest of these is love

Hosana Mwana wa Daudi

Kisha wakamleta huyo mwana punda kwa Yesu na kutandika mavazi yao juu yake, naye akampanda. Watu wengi wakatandaza mavazi yao barabarani na wengine wakatandaza matawi waliyokuwa wamekata mashambani.

Kisha wale waliokuwa wametangulia mbele na wale waliokuwa wakifuata nyuma wakapaza sauti, wakisema,

Hosana! Amebarikiwa Yeye ajaye kwa Jina la Bwana!

Umebarikiwa Ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi!

Hosana kwake Yeye Aliye Juu!

Marko 11:7:11

Palm Sunday - Matawi

Omba siku zote

Mpendwa, 

Mungu anasikia ombi lako na wala hupaswi kuacha kuomba , kwani Mungu hufanya kwa wakati unaofaa, ingawa unaweza ona kuwa anachelewa, lakini omba usiache, Yesu anasema “…imewapasa kumwomba Mungu siku zote wala wasikate tamaa” Luka 18:1. Mungu atawasikiliza na kuwapatia “… haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku…” Luka 18: 7 , hivyo omba bila kuchoka kama yule mama mjane aliyekuwa alyekuwa anadai haki yake.. Luka 18:2-8.

Tuombe:

Mungu wa milele , Nakushukuru kwa yote unayonijalia kwa kadiri ya upendo wako, nipe leo nguvu za kuomba bila kukata tamaa. Amen.

Omba Bila Kuchoka
Luka: 18:1-8 : Usikate tamaa omba

Mungu anasamehe na anaondoa hukumu zako,

Mpendwa,

Moyo u radhi lakini mwili ni dhaifu, Mungu anatupenda na anatusamehe kila tunapomwomba radhi, na hufuta hukumu zote kama tukitubu kweli kutoka moyoni. “Bwana ameziondoa hukumu zako, amemtupa nje adui yako. Mfalme wa Israel, naam , yeye Bwana , yu katikati yako, hutaogopa uovu tena.” Sefania 3:15

Tuombe: Mungu wa milele, asante kwa kuondoa hukumu zangu, nipe neema zako nisirudi tena dhambini. Amina

Lishike Neno na utakuwa huru

Mpendwa katika Kristu,

Mungu anakupenda sana, na ndiyo maana kila siku anakukumpusha umkumbuke yeye na ukimkumbuka na kumwabudu atakuweka huru. Neno la Mungu ndilo funguo ya kukuweka huru. Katika Yohane 8:31-32 , Yesu anasema “Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli, tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru”

Mpendwa ukitaka kuwa huru, ifahamu kweli, na hiyo kweli inapatikana katika neno la Mungu.

Tuombe: Mungu Mwema wa milele, nipe nguvu ya kulitafakari neno lako kila mara ili niijuie ile kweli nipate kuwa huru. Amen