Tupendane

courtesy: hdwallpapers.in“Wapenzi na tupendane, kwa kuwa upendo watoka kwa Mungu. Kila apendaye amezaliwa na Mungu naye anamjua Mungu. Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni upendo”
1 Yohana 4: 7-8

Mtegemee Mungu atakusaidia

burdensMpendwa,

Ni fajara iliyoje kujua kwamba kuna Mungu wetu ambaye anakupa nafasi ya kumpa matatizo yako, ili mradi tu uwe mtoto wake kwa kut
enda na kufuata yale anayotaka , kwa hiyo siku zote ” Mtwike BWANA fadhaa zako, naye atakutegemeza, hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.” Zaburi: 55:22.

Tuombe. Bwana Mungu nipe nguvu ya kutenda mema ili niwe mwenye haki wako, na kupata nafasi ya kukupa shida zangu. Amina

Mshukuru Bwana, kwa maana ni Mwema…

Image Courtesy: funzug.comMpendwa;

Mungu wetu ni wa upendo na ni mwema sana yapaswa kumsifu na kumshukuru kwa mema mengi anayotujalia bila kujali shida ambazo pengine unazipata, yeye anajua na anatutunza, tumsifu, kama mzaburi asemavyo

“Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na katika nyua zake kwa kusifu, mshukuruni yeye na kulisifu jina lake. Kwa maana BWANA ni mwema na Upendo wake wadumu milele, uaminifu wake unaendelea katika vizazi vyote.”  Zaburi 100: 4-5

Tuombe: Mungu wa upendo Asante kwa wema wako.  Amina

” Basi kesheni ninyi kila wakati, mkiomba…”

courtesy image: http://chaplainsblog.tumblr.com/Mpendwa katika Kristo,

Siku ya Bwana yaja bila hodi, na Mungu anakupenda sana na anapenda siku hiyo ifikapo akakukute umejiandaa, na ndiyo maana Bwana Yesu anakukumbushaBasi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo; kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzaima. Basi kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika hayo yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.” Luka: 21:34-36

Tuombe: Mungu mwena nipe neema ya kutumia wakati na mambo ya dunia hii kujiadnaa na ujio wako. Amina

Mtumaini Mungu atafuta machozi yako,

Ndugu Mpendwa,

Japokuwa unaweza ukawa katika huzuni na kilio cha moyo, kutokana na taabu ya maisha , lakini usiache kumtumaini Mungu, kwani ni yeye pekee anaweza kukupitisha hapo na kukuweka mahali pa faraja , katika Ufunuo 21:4 biblia natuambia “Naye atafuta kila chozi katika macho  yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo , wala kilio , wala maumivu hayatakuwepo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita” , basi Mungu leo anafuta machozi yako, piga magoti na mwambie lililo moyoni mwako.

Amina

Mpe maskini na Mungu hataugeuza uso wake mbali nawe

Courtesy: http://blogs.tribune.com.pk/Mpendwa,

“Toa sadaka katika mali zako, wala utoapo sadaka jicho lako lisiwe na choyo; wala usiugeuzie uso wako mbali na mtu maskini, nawe hutageuziwa mbali na uso wa Mungu” Tobiti 4: 7. Hivyo ndigu,  leo Mungu anataka ufanye tendo la huruma kwa yule mhitaji utakaekutana naye, Fanya hivyo kupata baraka za Mungu aliye juu.

 Tuombe: Mungu mwema, asante kwa siku ya leo , wape wale wahitaji neema ya kuyapata watayoyatamani, nipe nami nguvu za kuwa mtoaji kwa wahitaji. Naomba nakushukuru kwa Jina la Mungu wetu wa Mbinguni, Amina.