Upendo

Mpendwa,

Leo ni Alhamisi Takatifu au Alhamisi Kuu (Maundy Thursday, Holy Friday, Great Friday), siku ambayo Yesu alionyesha upendo mkuu kwa wanafunzi wake, ni upendo usiopimika, na ni upendo ambao anauonyesha kwako pia , mpende na mwamini  Yesu na usimsaliti kama alivyofanya Yuda.

Tunasoma upendo wa Yesu katika Yohana 13:1-11 ” Ilikuwa siku moja kabla ya sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua ya kuwa wakati wake wa kuondoka duniani na kurudi kwa Baba yake umekaribia. Alikuwa amewapenda sana wafuasi wake hapa duniani, akawapenda hadi mwisho. Na wakati alipokuwa akila chakula cha jioni pamoja na wanafunzi wake, shetani alikuwa amekwisha kumpa Yuda Iskariote, mwana wa Simoni, wazo la kumsaliti Yesu.  Yesu akijua ya kwamba Baba yake alikwisha mpa mamlaka juu ya vitu vyote; na kwamba yeye alitoka kwa Mungu na alikuwa anarudi kwa Mungu, alitoka mezani akaweka vazi lake kando, akajifunga taulo kiunoni. Kisha akamimina maji katika chombo akaanza kuwaosha wanafunzi wake miguu na kuikausha kwa ile taulo aliyojifunga kiu noni.  Alipomfikia Simoni Petro, Petro akamwambia, “Bwana, wewe unaniosha miguu?”  Yesu akamjibu, “Hivi sasa huelewi ninalofa nya lakini baadaye utaelewa.”  Petro akamjibu, “La, hutaosha miguu yangu kamwe!” Yesu akamwambia, “Kama sitaosha miguu yako, huwezi kuwa mfuasi wangu.”  Ndipo Petro akasema, “Kama ni hivyo Bwana, nioshe miguu yangu pamoja na mikono yangu na kichwa changu pia!” Yesu akamwambia, “Mtu aliyekwishaoga ni safi mwili mzima naye hahitaji tena kunawa ila kuosha miguu tu. Ninyi nyote ni safi, isipokuwa mmoja.” Yesu alifahamu ni nani angemsaliti, ndio sababu akasema, “Ninyi nyote ni safi, isipo kuwa mmoja.”

Tuombe:

Mungu wa milele nipe neema za kukupenda wewe siku zote, naomba nakushukuru kwa Jina la Yesu mwanao. Amina

Holy ThursdayHoly Thursday-1

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s