Usalipo Amini unayapokea

Mpendwa,

Imani katika kila sala uisaliyo ni muhimu sana, unaweza kuwa unaomba sana, lakini huoni, matokeo ya sala yako, je unaamnini kuwa unayapata unayoomba, Yesu anasema “Kwa sababu hiyo nawaambia: Yeyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu” Marko 11:24. Tunaona hapa hasemi “mtayapokea” bali mnayapokea, kwa hiyo, ukiamini,  ni kitendo cha hapo hapo, Mungu anapenda sana upate unayotamani, kikubwa ni kufanya moyo wako kuwa safi, tubu dhambi, samehe waliokukosea, omba na amini, nawe yote uliiomba yatakuwa yako.

Tuombe

Mungu wa mbinguni, nisaidie kila niombapo, nisione shaka moyoni mwangu, ili niyapokee niombayo. Amina

Nitafanya njia hata jangwani

nitafanyanjia jangwaniKuna wakati, unajikuta huna cha kufanya kutokana na mazingira magumu ya shuguli na majukumu ya kila siku, je upo katika wakati kama huo, una mgonjwa lanini huna uwezo wa kumhudumia, una familia lakini una wakati mgumu wa kuwapa mkate wa kila siku, unafanya kzi lakini mahali pako pa kazi hapana Amani, mkumbuke na mwombe Mungu leo, kwani Mungu ni mwenye huruma na mwaminifu, hapendi tutazame ya kale bali tumwangalie Yeye na atafanya njia.  Leo Mungu anasema

“Msiyakumbuke mambo ya kwanza,

wala msiyatafakari mambo ya zamani!

Tazama nitatenda neno jipya:

sasa litachipua je, hamtalijua sasa?

Nitafanya njia hata jangwani,

na mito ya maji nyikani” Isaya 43:19

 Tuombe:

Mungu wa milele, fanya njia katika jangwa la majaribu nipitialo, na mito katika nyika ya matatizo niliyonayo . Amina

“…nitawapa kinywa na hekima..”

Mpendwa, 

Mungu siku zote hutuongoza katika kuongea yanayofaa, ni vema kabla hujaongea kutafakati, ili unakachozungumza kiwe ni chema mbele za Mungu na watu, ukijipa moyo na kumtanguliza Mungu kabla ya kuongea, Mungu wetu ni mwema atakupa maneno ya hekima yanayofaa kuzumgumza “ kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga” Luka 21:15

Basi mwombe Mungu wakati unapokuwa katika hali ya kutaka kujibu hoja yoyote katika maisha, usiwe na jazba wala tusihofu ni jibu gani tutakalotoa, kwani Mungu atakupa hekima.

Jipe moyo, kwa Mungu yote yanawezekana

Bali Kwa Mungu yote yanawezekanaYesu anatuhakikishia kwamba hakuna jambo lolote hapa duniani ambalo Mungu hawezi kulifanya, Mungu ni mkuu na anaweza yote. Mpendwa katika maisha yetu Mungu anapenda kutuokoa katika mambo mbali mbali tunayopitia ambayo yanatupa wakati mgumu sana. Je una huzuni sana, je umeumizwa sana, je unapitia wakati mgumu kiuchumi, Leo Yesu , kama alivyoowaambi wanafunzi wake walipoomuliza , “ Ni nani basi awezaye kuokoka” , anasema  “… kwa mwanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo, maana yote yanawezekana kwa Mungu” Marko 10:27,  ndiyo maana ndugu nakwambia leo ni siku yako mpya, mtumani Mungu, tunajuwa kwamba ili dhahabu ing’ae ni lazima ipite kwenye moto, basi yawezeka bado kitambo kidogo tu nawe utang’aa na yote yatapita, Mwombe Mungu sana, kwani yote  Kwake yanawezekana.

Amani iwe kwenu , Pokeeni Roho Mtakatifu

Holy-Spirit-DoveIkawa jioni ya ile siku ya kwanza ya juma, wanafunzi Wake walipokuwa pamoja, milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi, Yesu aliwatokea, akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi.’’

Baada ya kusema haya, akawaonyesha mikono Yake na ubavu Wake. Wanafunzi Wake wakafurahi sana walipomwona Bwana. Yesu akawaambia tena, “Amani iwe nanyi! Kama vile Baba alivyonituma Mimi, Mimi nami nawatuma ninyi.’’

Naye alipokwisha kusema haya, akawavuvia, akawaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu. Mkimwondolea mtu ye yote dhambi zake, zitaondolewa na ye yote mtakayemfungia dhambi zake, zitafungiwa. Yohana 20:19-23

Wanyofu wa watauona uso Bwana,

Ndugu Mpendwa,

Mungu baba anapenda tuwe wanyofu ili tuweze kufika kwake mbinguni na kuuona uso wake. Unapokuwa mwovu Mungu anakupatiliza na kukupa adhabu, kama mzaburi asemavyo “ Juu ya waovu atawanyeshea makaa ya moto mkali na kiberiti kinachowaka, upepo wenye joto kali ndio fungu lao. Kwa kuwa BWANA ni mwenye haki, hupenda haki, watu wanyofu watauona uso wake” Zaburi 11:6-7.
Hivyo basi tuombe neema ya kumtumikia Mungu daima, na njia ya kuwa wanjofu ni kuzishika amri zake.

Mungu hatawaacha wala hatawatupa ninyi

Courtesy: http://revandy.org/Mpendwa,

Bwana Mungu anatualika leo tusiogope kwa jambo lolote lile, yaweza ukawa katika hali ngumu ya majonzi ama wasi wasi kutokana na mambo mbali mbali au pengine mtu fulani anakupa wakati mgumu katika maisha yako, yote hayo Mungu atayaweka sawa, Mungu atakupigania , unachopaswa kufanya kushika mkono wa Bwana kwa sala  na kumtumainia Yeye. Basi Mungu leo anakualika kwa kusema “Iweni imara na moyo wa ushujaa. Msiogope wala msifadhaike kwa sababu yao, kwa kuwa BWANA Mungu wenu anakwenda pamoja nanyi, kamwe hatawaacha wala hatawatupa ninyi” Kumbukumbu la Torati 31:6

 Tuombe:

Mungu wa milele, Mungu wa Mbinguni, tazama mimi mwanao nakuja mbele zako nikileta furaha, huzuni na masumbuko yangu kwako, nipe moyo mkuu, natumaini kuwa upo nami siku zote, asante kwa sababu hujaniacha wala kunitupa. Amina