Ee Mungu uniokoe kwa jina lako, unitetee kwa uwezo wako.
Ee Mungu, sikia maombi yangu, usikilize maneno ya kinywa changu.
Wageni jeuri wananishambulia, na watu wakatili wanatafuta maisha yangu
watu wasiomjali Mungu.
Hakika Mungu ni msaada wangu, Bwana ndiye anayenitegemeza.
Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia,
kwa uaminifu wako uwaangamize
Nitakutolea dhabihu za hiari,
Ee BWANA, nitalisifu jina lako kwa kuwa ni vema.
Kwa maana ameniokoa kutoka katika shida zangu zote,
macho yangu yameona kwa furaha ushindi dhidi ya adui zangu
Zaburi 54
Advertisements
Nimependa huduma yenu ,,Mungu awabariki sana
Amina
HUDUMA YENU NI NJEMA SANA MUNGU AWABARIKI
mbarikiwe sana