Uniongoze katika kweli yako ee Bwana

Mpendwa,
Amani ya Mungu baba na upendo wa Bwana Yesu vikae nawe;
Leo Mungu anapenda kukupa uongozi wake  katika ufanyayo. Kuna nyakati ambapo unakuwa huna suluhishi katika jambo fulani unalotaka kulitatua, huoni ufanye nini , basi ukiwa katika hali kama hiyo, omba uongozi wa Mungu, naye atakuonyesha njia, Sali sala hii fupi toka Zaburi 25:5; “Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa” na Mungu wetu ni mwema sana atakupa maongozi yake.

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu

Mendwa,

Bwana na awe nawe siku hii,

Kuna wakati faraja inakuwa imepotea katika maisha, Na hasa tunapokuwa Na mateso, yaweza ikawa ya ugonjwa au mahusiano au lolote. Unaweza ukajiona huna tumaini; mateso na matatizo yanakuwa yaunguruma kama radi ama simba katika maisha yako. Mpendwa “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.” Zaburi 46:1-3, Hivyo Hakuna lisilowezekana kwake Mungu, basi piga magoti leo mwombe Mungu, mwambie yote, naye atakuvusha katika mateso yote.

Sala ya Baraka

Bwana unibarikie, na kunilinda;
Bwana uniangazie nuru za uso wako, na kunifadhili;
Bwana uniinulie uso wako, na kunipa amani.
Unipelekee msaada toka patakatifu pako, Na kunitegemeza toka Sayuni.
Uzikumbuke sadaka zangu zote, Na kuzitakabali dhabihu zangu.
Unijalie kwa kadiri ya haja ya moyo wangu, Na kuyatimiza mashauri yangu yote.
Amina

Hesabu 6: 24-26, Zaburi 20: 2-4

 courtesy: http://www.sodahead.com/
God Bless You

Mtwike Bwana Mzigo wako

Courtesy: http://www.thegardenworshipcenter.com
Psalms 55:22

Mpendwa,

Upenda wa Bwana na uwe nawe ,

Je mpendwa una swala ambalo unashidnwa kupata mwafaka wake, liwe la maisha au la kiroho? Habari njema leo ni kuwa yupo ambaye anweza kukusaidia mzigo wako; “Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele” Zaburi 55:22

Basi ndugu, piga magoti, mwombe Mungu akusaidie katika yake yaliyo mzigo kwako, lililo kuu ni kuwa mtu wa haki na kutenda mema, kwani ukiwa mwenye haki ndipo Mungu hatakuacha.

Tuombe: Mungu wa milele, asante kwa kuwa wewe hujaniacha, pokea mizigo yangu. Amina

Amani nawaachieni…

Mpemdwa,
Je, umekosa amani ndani ya moyo wako, au ndani ya familia yako, ama sehemu yako ya kazi?, usiogope, Mungu anakupa zawadi ambayo huwezi kuipata katika ulimwengu huu, AMANI, Yesu anasema “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga” Yohana 14:27. Basi mpendwa usiwe na hofu kwa yote yanayotokea katika maisha yako, jipe moyo na Mungu atakupa amani.
Tuombe: Mungu Baba , ulisema tushukuru kwa kila jambo, nasema asate kwa kila jambo linalotokea katika maisha yangu, nipe Amani, nakutumanini wewe. Amina

Maneno ya hekima – Mwenye kufunua siri huivunja amani

Mpendwa,

“Mwenye kufunua siri huivunja amani, wala hatapata rafiki wa nafsi yake. Umpende rafiki yako, na uwe mwaminifu kwake; walakini ukizifunua siri zake , usifuate nyuma yake; kwa maana kama mtu kumharibu adui yake, wewe umeharibu urafiki wa jirani yako. Kama ndege uliyemwachilia mkononi mwako, umemwacha jirani yako, wala humpati tena; usimfuate amekwenda zake mbali, umeokoka kama paa mtegoni. Mradi jeraha itakuja kufungwa , hata baada ya mashutumu kuna mapatano; bali mwenye kufunua siri hata tumaini. “

Yoshua bin Sira 27:16-21

Tumia karama yako kwa kadiri Mungu alivyokujalia

Mpendwa, Amani ya Kristo iwe pamoja nawe,
Kila mmoja ameubwa kwa dhumuni maalumu hapa duniani, Mungu anakupatia kitu Fulani ili kikusaidie wewe na umsaidie mwingine kwa hicho ili kufika mbinguni, kwa neema na kipaji ulichonacho hakikisha unakitumia vema ili jina la Mungu litukuzwe na sote tufike kwake mbinguni “Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha” Warumi 10: 6-8.
Mpendwa mwombe Roho Mtakatifu, utambue karama yako na kuitumia kwa mapenzi ya Mungu.