Heri mtu yule amchaye Bwana,

Mpendwa,
Baraka za Mungu wetu na ziwe nawe.
Mara nyingine umekuwa ukijiuliza ni kwanini una maisha uliyonayo,  pengine unaona kama vile Mungu amekubariki sana au anakupa adhabu, kwamba huna maendeleo, na kila unalofanya halifanikiwi, na hata wale ndugu na jamaa zako, na hata watoto wako hawafanikiwi, unaweza jiuliza ni kwa nini  haya yote ayanatokea? Mungu anakupenda sana na anataka uwe na maisha mazuri yenye baraka nyingi,  si kwa wewe tu bali watoto wako na kizazi chako pia. Basi ufanye nini sasa, mpendwa ili upate Baraka toka kwa Mungu, unatakiwa kuacha dhambi zote na  kumcha Yeye na kumtumikia siku zote, ukimpendeza Mungu katika matendo na maisha yako,  Mungu wetu ni mwema sana  atakupa Baraka, wewe na kizazi chako chote, Mzaburi anatuambia “Haleluya. Heri mtu yule amchaye Bwana, Apendezwaye sana na maagizo yake.  Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.  Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele.” Zaburi 112:1-3
Mpendwa, mche Mungu, ubarikiwe
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s