Bwana ni mwaminifu, atakulinda na Mwovu

Mpendwa,

Amani ya Bwan iwe juu yako,

Leo neno linatukumbusha kuwa Bwana Mungu ni mwaminifu kwetu na anatulinda na adui mwovu. Umempokea Yesu na unajitahidi kadiri ya neema za Mungu kufuata amri za Mungu na kutenda yaliyo mema, hilo ndilo muhimu, lakini shetani hapendi hata siku moja tumwelekee Mungu, kwani anajua tukiwa wana wa Mungu basi tupo njiani kwenda kumwona, na yeye shetani hatakuwa na chake, na hivyo atafanya kila njia kuhakikisha unatoka katika mstari ulio njooka, “Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu.” 2 Wathesalonike 3:3

Basi tumtumaini Mungu, kwani kwa neema zake anatuepusha na kutulinda na yule mwovu, tusiogope kutenda mema wakati wote.

Heri mtu yule ambaye haendikatika shauri la watu waovu

Mpendwa,

Uovu ni mwingi hapa duniani, na tunaishi katika maisha ambqyo tunaweza tukashawishiwa kutenda uovu kutokana na mazingira tunayokuwa , lakini je unafanya juhudi gani kuepuka uovu na aina zote za dhambi?, Mungu leo akupa ahadi njema kama ukiishi katika njia njoofu isiyo ya uovu. utapata furaha na baraka, Mungu atakufanikisha katika kila jambo endapo tu utaacha dhambi na kuachna na watu  wavou, neno linatumabia “Heri mtu yule ambaye haendikatika shauri la watu waovu,Wala hafuati njia ya wenye dhambi au kukaa katika baraza la wenye mizaha. Lakini huifurahia sheria ya BWANA, nayo huitafakari mchana na usiku. Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando yavijito vya maji,ambao huzaa matunda yake kwa majira na majani yake hayanyauki. Kila afanyalo hufanikiwa. Zaburi 1: 1-3.

Basi mpendwa acha dhambi za aina zote, kaa katika kutenda mema, kusaidia ndugu, yatima, kufanya kazi kwa bidii na Mungu atakusitawisha kama vile mmea ulio kando kando ya mto ambao maji hayapungui na unakuwa unashamiri siku zote.

Hakuna cha kututenga na upendo wa Mungu

Mpendwa,

Mungu ni mwenye upendo, ingawa tunaweza tukawa tuna huzuni wakati fulani kutokana na hali ya maisha “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.” Warumi 8:37-39

Msifanye wema wenu machoni pa watu

Mpendwa

Utoapo , mtolee Mungu kwa moyo na dhamiri iliyo safi. Yesu anasema “Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.” Matayo 6:1-4

Usigope

Mpendwa,

Leo Yesu anatupa nguvu ya kuendelea mbele katika maisha  bila kujali vikwazo mbele yatu, yaweza ikawa katika maisha  ya kimwili au kiroho, “Naye akawaambia, Ni mimi, msiogope. ” Yohana 6:20, aliwwambia wanafunzi wake wasiogope , nasi leo anayumbia, katika dhoruba yoyote ile ya maisha tusiogope, tumtumainie Yeye naye anatatuvusha pale tulipo.

Amina

Bwana, moyo wangu hauna kiburi

Mpendwa,

Jiachie kwa Bwana kwa kila hali naye atakulinda na kukuongoza “Bwana, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala na mambo yashindayo nguvu zangu.  Hakika nimeituliza nafsi yangu, Na kuinyamazisha. Kama mtoto aliyeachishwa Kifuani mwa mama yake; Kama mtoto aliyeachishwa, Ndivyo roho yangu ilivyo kwangu. Ee Israeli, umtarajie Bwana, Tangu leo na hata milele.” Zaburi 131