Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe.

Mpendwa,

Mbali ya kumwomba Mungu, kila wakati, tunapaswa  vilevile kusifu na kumshangilia kwa mema yote anayotujalia.

“Enyi watu wote, pigeni makofi, Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe. Kwa kuwa Bwana Aliye juu, mwenye kuogofya, Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote. Atawatiisha watu wa nchi chini yetu, Na mataifa chini ya miguu yetu. Atatuchagulia urithi wetu, Fahari ya Yakobo ambaye alimpenda. Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, Bwana kwa sauti ya baragumu. Mwimbieni Mungu, naam, imbeni; Mwimbieni mfalme wetu, naam, imbeni. Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote, Imbeni kwa akili. Mungu awamiliki mataifa, Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu. Wakuu wa watu wamekusanyika, Wawe watu wa Mungu wa Ibrahimu. Maana ngao za dunia zina Mungu, Ametukuka sana.” Zaburi 47courtesy: http://moreenn.blogspot.com/

Sisi tu watoto wa Mungu;

Mpendwa, Amani ya Bwan na iwe nawe.

Mateso huwa yanakuja katika maisha yetu na hatuwezi kuyazuia. Unapopata mateso yawe ya kimwili au ya kiroho, mtumaini Mungu, kwani kuteswa pamoja na Kristu ni Mwanzo wa kuurithi ufalme wa Mungu. Wewe ni mwana wa Mungu na roho anahsuhudia hivyo na kwa kuwa u mwana wa Mungu basi unapana urithi pamoja na Kristu “Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.” Warumi 8:16-18

Basi Mpendwa tumwombe Mungu atupe nguvu ya kuvumilia mateso kwani ni mwanzo wa kuurithi ufalme wa Mungu.

Tumshukuru Mungu..

Mpendwa,

“Ni neno jema kumshukuru Bwana, Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu. Kuzitangaza rehema zako asubuhi, Na uaminifu wako wakati wa usiku.” Zaburi 92:1-2 “Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi. Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.” Zaburi 95:2-3

Asante Mungu kwa amani na utulivu, zidi kutupa neema na mwongozo wako. Amina

7. Itafute amani

Mpendwa,

“…mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;  watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka. Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila.Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana.” 1 Petro 3:8-11