Ee Bwana, unijulishe njia zako

Ee Bwana, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako, Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa. Bwana yu mwema, mwenye adili, Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia. Wenye upole atawaongoza katika hukumu, Wenye upole atawafundisha njia yake. Njia zote za Bwana ni fadhili na kweli, Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.Siri ya Bwana iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake.

Zaburi 25:4-5,8-10,14

Mtafute Yesu kwa kila mbinu

Mpendwa,

Baraka na Neema za Mungu wa mbiguni ziwe juu yako.

Unapokuwa unataka kufanikiwa katika maisha ni lazima ufanye juhudi katika kazi na kutafuta mbinu mbali mbali ili utimize lengo ulilonalo, hivyo ndivyo maisha yetu ya kila yalivyo. Kwa upande mwingine ili uweze kufanikiwa kiroho ni lazima kumtafuta Yesu, naye atakuja kwako. Simulizi la Zakayo linatufundisha jambo hili la kutumia kila mbinu kumtafuta Yesu, Zakayo kwa kuwa alikuwa mfupi lakini alikuwa na hamu ya kumwona Yesu, hivyo akapanda juu ya mkuyu, na Yesu kwa kuona juhudi zake, akamwita na kushinda ndani mwake siku hiyo, neon linatuambiaNa tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri. Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo. Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile. Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako. Akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha. Luka 10:2-6

Basi mpendwa tuwe na moyo wa kuopanda juu ya mkuyu ili kumtafuta Yesu, kupanda mkuyu ni kuwa watu wa maombi, sala, majitoleo na matendo mema, kwa namna hiyo Yesu atakuja na kushinda ndani ya roho zetu.

Barikiwa sana.

Hurmianeni na kupendana

Mpendwa,

ukimvumilia na kumhurumia mwenzako utairithi baraka ” …mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu; watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka. Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila. Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana. Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya” 1 Petro 3:8-12

Mke Mwema Hufumbua kinywa chake kwa hekima

“Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani. Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.  Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake. Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo. Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali. Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao. Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake”  Mithali 31:10-15, 26

courtesy: http://www.daphnebazaar.com/product/daphne-gold-plated-flower-ring-with-american-diamonds-best-for-gift/

Jivikeni upendo

Mpendwa,
Kuwa mkamilifu ni kazi kubwa sana, na unatakiwa kujitoa kweli kweli ili kuwa mkamilifu, na namna ya mojawapo inayoweza kukusaidia kuwa mkamilifu ni kuwa na upendo, neno linasema “ Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu” Wakolosai 3:14, kwa upendo unakuwa unawafanyia na unafanya mambo yote kama inavyotakiwa. Basi mwombe Mungu akupe nguvu ili kuweza kuwa na upendo utakaosaidi kuwa na ukamilifu.

Mpende adui yako

Mpendwa,

“Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,  ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? “ Matayo 5:43-46

love-your-enemies

Asiyetenda haki hatokani na Mungu

Mpendwa,

Amani ya Bwana na iwe juu yako.

Upendo ni kitu muhimu katima maisha yetu, kwani tukiwa na  upendo  tutawatendea ndugu zetu na wenzentu yaliyo mema, ukimpenda mtu huwezi kumsengenya, kumwibia, kumtakia lolote baya au hata kumshawishi kutenda maovu, mtu unaempenda utamtakiwa mema na amani tu. Ukiwa na upendo utaitwa mtoto wa Mungu na shetani atakuwa mbali nawe, kwa matendo yako utatambulikana kuwa wewe ni wa Mungu au shetani , neno linasema “ Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.” 1 Yohana 3: 10.

Basi Mpendwa, mwombe Roho Mtakatifu, akupe neema ya kuwa na upendo kwa watu wengine, pale ambapo unaona ndugu kakosa upendo uwe wa kwanza kusema ukweli kuliko kuficha moyoni.

“Ee Bwana unifanye niwe chombo cha amani yako, palipo na chuki nilete mapendo” Amina

Njoni, tuabudu, tusujudu

Mpendwa,

Mungu wetu ni mwema natatupatia kila kitu, na ameunmba vitu vingi na almetuumba nasi pie ahivyo ni veyma kuwambudu Yeye aliye mkuu kuliko vyote “Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba. Kwa maana ndiye Mungu wetu, Na sisi tu watu wa malisho yake, Na kondoo za mkono wake. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!” Zaburi 95:6-7

courtesy: https://www.pinterest.com/pin/9007267978503044/