beautiful_merry-_christmas-_images

Sikiliza Sauti ya Mungu na itii

“Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.   Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.  Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,  Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.  Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe;  asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.

Matayo 1:18-25

Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako

Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako, Utupe wokovu wako.
Na nisikie atakavyosema Mungu Bwana, Maana atawaambia watu wake amani, Naam, na watauwa wake pia, Bali wasiurudie upumbavu tena.
Hakika wokovu wake u karibu na wamchao, Utukufu ukae katika nchi yetu.
Fadhili na kweli zimekutana, Haki na amani zimehusiana.
Kweli imechipuka katika nchi, Haki imechungulia kutoka mbinguni.
Naam, Bwana atatoa kilicho chema, Na nchi yetu itatoa mazao yake.
Haki itakwenda mbele zake, Nayo itazifanya hatua zake kuwa njia.

Zaburi 85:3-13

Ee Bwana, unijulishe njia zako,

Ee Bwana, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako, Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa. Ee Bwana, kumbuka rehema zako na fadhili zako, Maana zimekuwako tokea zamani.  Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, Wala maasi yangu. Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee Bwana kwa ajili ya wema wako. Bwana yu mwema, mwenye adili, Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia. Wenye upole atawaongoza katika hukumu, Wenye upole atawafundisha njia yake.

Zaburi 25:4-9

Hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.

Mpendwa,

Yesu anatuma wanafunzi wake kwenda kila mahali kuhubiri injili na anwaambia  “Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.” Matayo 10:6=7

Kwanza katika kipindi hiki cha maajilio tunakumbushwa kuwa ufalme wa Mungu umekaribia, na ufalme wenyewe ni Yesu anapozaliwa wakati wa Noeli/Kristimasi, hivyo tujiandae , kwa kuacha dhambi na yale mambo ambayo Mungu hapendi tusafishe roho zetu kabla ya kumpokea Masiha

Mbili baada ya kujiandaa sisi wenyewe, ni lazima twende kuwahubiria wengine ufalme huo kama vile mitume walivyofanya, hivyo tunatumwa kwenda kila mahali kuhubiri; tuhubiri katika jumuiya zetu, familia zetu, mahali pa kazi pia na sehemu zote kwa kila mtu.

Ubarikiwe

Zikiliza Amri, utafanikiwa

Mpendwa

Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata. Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari;  Tena wazao wako wangalikuwa kama mchanga, na hao waliotoka katika tumbo lako kama chembe zake; jina lake lisingalikatika, wala kufutwa mbele zangu.” Isaya 48:17-19

Haleluya. Msifuni Bwana;

“Haleluya. Msifuni Bwana; Maana ni vema kumwimbia Mungu wetu, Maana kwapendeza, kusifu ni kuzuri. Bwana ndiye aijengaye Yerusalemu, Huwakusanya waliotawanyika wa Israeli. Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuziganga jeraha zao. Huihesabu idadi ya nyota, Huzipa zote majina.
Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu, Akili zake hazina mpaka.
Bwana huwategemeza wenye upole, Huwaangusha chini wenye jeuri.”

Zaburi 147:1-6