mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.” Waefeso 4:22-24

MWAKA MPYA UNAKUPA MWANZO MPYA. MUNGU AKUFANIKISHE KATIKA MWAKA MPYA.

SAMAKI

Mto ule ule ambao Petro na wenzake  walihangaika usiku kucha bila kupata samaki , ndiyo katika mto huo huo , walivua Samaki wengi asubuhi yake waliokuwa wamekutwa na Yesu.

Swala kubwa hapa ni kwamba, Yesu alipowakuta akina Petro pale mtoni asubuhi ile aliwaambia Mna samaki? , Wakajibu  Hapana (Yohana 21:5-6). Baada ya hapo Yesu, hakusema wabadilishe waende kwenye mto mwingine kuvua samaki, bali aliwaambia  watupe nyavu zao kwenye kina kikubwa cha mto ule ule ili wapate samaki.

Yawezekana katika mwaka 2016 umejaribu sana kuvua samaki lakini hujapata kitu, hukupata kazi, hukupata mchumba, hukuwa na kipato kizuri, hukupata watoto, hukuwa na Amani, mwaka ulijaa magomvi, vita na chuki, hukuwa na mafaniko yoyote uliyotegemea. Ndugu, unapoona maisha hayendi kama ulivyotarajia, huo si wakati wa kubadili mto ili kupata samaki, sio wakati wa kutafuta kazi ingine, au kuhamia kanisa lingine, au kubadili mwenza wako (mke au mume) na kwenda kwa mwingine, La..

Kikubwa ni kutupa nyavu zako kwenye kina kirefu cha mto, Yaani kuongeza imani yako kwa Mungu, ongeza urafiki wako na Yesu, ukiamini kuwa Mungu atakupa yote, atakuponya, atakuongezea tumaini, atakupa kazi mpya, atakupa mahusiano mapya na atakupa Baraka na kukubariki katika kila jambo, Omba, Sali, Amini, utapata.

Mungu akupe Baraka ili uweze kurusha vyavu zako kwenye Kina kirevu cha Imani kwa Mungu , ili mwaka  2017 uvue samaki wengi Zaidi.

UBARIKIWE

courtesy: WhatsApp

Kwanini kuomba wakati Mungu anajua?

Mpendwa,

Ulishawahi kujiuliza kwa nini unaomba wakati Mungu anajua hata kabla hujaomba? Neno linasema “Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.” Isaya 65:24, tena Yesu mwenyewe anasema “Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.” Matayo 6:8

Kwanza napenda kukupa moyo usiache kuomba kwani Baba Mungu Mwenyezi ameshakuhakikishia kuwa anajua na kuyajibu maombi yako, siku zote dumu katika sala na kuomba. Mungu anataka uombe ingawa anajua unachotaka kwani anataka kuona unyeyekevu wako “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake” 1 Petro 5:6, anapenda asikie ukitamka mwenyeywe matakwa yako kutoka katika kinywa chako, hivyo Mpendwa kuwa mnyeyekevu na enenda mbele zake na kusema bila woga mahitaji yako yote, naye kwa kuwa ameshayajua unayohitaji atakupatia.

Ubarikiwe na Bwana

Hope
Courtesy: http://greatergood.berkeley.edu/

Usichike Kungoja…

Mpendwa,

Usishahau “… neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba” 2 Petro 3:8-9, hivyo basi lolote unaolomwomba  Mungu, kumbuka lipo katika kapu lake na hajasau , atakupa kwa wakati wake.

Ubarikiwe

Kufuata Sheria ni Kufanikiwa

Heri ni neno linalomaanisha, uzuri au jambo jema; Mpendwa unapofuata sheria (za Mungu na za Wanadamu) unapata heri yaani unapata baraka toka kwa Mungu na mambo yako yanakwenda vizuri, ndiyo maana mzaburi anasema “ Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya Bwana.  Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote.” Zaburi 119:1-2, basi fanya bidii kuzifuata njia za Bwana. Ili kupata heri unapaswa kufanya bidiii kuacha dhambi na kufundishwa na Bwana “ Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. Ee Bwana, umehimidiwa, Unifundishe amri zako.” Zaburi 119:11-12. Fanya bidii huku ukiomba Mungu akutendee mema , akupe nguvu kulitii neno lake ambalo ndiyo sheria yenyewe “Umtendee mtumishi wako ukarimu, Nipate kuishi, nami nitalitii neno lako.  Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako. “ Zaburi 119:17-8.

 Ubarikiwe