Usirudi Nyuma

“Ndipo Bwana akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa Bwana. Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile. Lakini mkewe Lutu akatazama nyuma yake, akawa nguzo ya chumvi.”

Mwanzo 19:24-26

Kuwa Mnyenyekevu

Mpendwa,

Ni vema kuwa wanyenyekevu wakati wote , kwani kwa kufanya hivyo ni rahisi  kuurithi ufalme wa Mungu. Yesu “akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.  Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.  Na ye yote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi;  bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.” Matayo 18:3-6

Mungu akubariki na akupe unyeyekevu

Mpendwa,

“Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo,  ya kwamba waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu. Watu hao ndio waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho. Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,  jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.” Yuda 1:17-21

 

 

Mungu Hachoki, usiache kumwomba

Mpendwa,

“Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.  Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.  Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka;  bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.” Isaya 40:28-31