“Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako. Niletewe nuru yako na kweli yako ziniongoze, Zinifikishe kwenye mlima wako mtakatifu na hata maskani yako. Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliye furaha yangu na shangwe yangu; Nitakusifu kwa kinubi, Ee MUNGU, Mungu wangu”

Zaburi 42:2-3; 43:3-4

Mpendwa,

Yesu leo anatuambia ” Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.  Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake. Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe.  Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza wakawatenda vile vile. Mwishowe akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu.  Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake.  Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua.  Basi atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawatendaje wale wakulima?  Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake. ” Matayo 21: 33-41

Mpendwa jilize, je na mimi ni kama watumwa hawa?

Ubarikiwe.

Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote

Neno la Faraja

Mpendwa,

Leo tumenza kipindi kingine katika mwaka cha kujitakasa na kumrudia Mungu, kipindicourtesy: http://www.ruts.org/devotions/a-heart-of-repentance/ cha Kwaresma. Kwa ishara ya nje Mfalme wa Ninawi aliketi katika majivu ili kutubu dhambi (Yona 3:6), leo mbali ya baadhi kujipaka majivu, lakini lililo kuu ni ishara ya ndani ya kumlilia Mungu na kuacha dhambi na mabaya yote (Yona 6:8). Kipindi hiki ni kumwomba Mungu kwa neema zake kuacha mabaya na kutenda mema, na kuyaendeleza hayo mema hata baada ya kipindi cha Kwaresma kwisha.

Basi tunakumbushwa mambo makubwa manne

  1. Kumrudia Mungu; kutubu na kuacha udhalimu wa kila aina , uonevu, usengenyaji, uzinzi, rushwa, uongo na dhambi zote; Mungu ni Mwenye Huruma atatusamehe.
  2. Kutoa kwa moyo bila kujionyesha; ili kuwasaidia wale wahitaji,; wagonjwa, wajane, walemavu, yatima na kila tunayemwona ni mwitaji.
  3. Kusali kwa moyo; na kuomba bila kujionyesha kuwa tunajua kusali, bali kupata muda maalumu ya kusali kwa siri na kuomba, kujiombea sis wenyewe na kuwaombea wengine.

View original post 299 more words

Bwana ndiye mchungaji wangu

Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.

Zaburi 23

Psalm 23, The Lord is my Shepherd. Courtesy : YouTube

Ombeni, nanyi mtapewa

Mpendwa,

Mungu baba ni mwema sana na haachi kutupa pale tunapomomba, hivyo usikate tamaa hata kama umetumia muda mrefu kuomba, endelea kuomba. Yesu anasema “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;  kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?” Matayo 7:7-8,11

courtesy: http://www.creativewallquotes.com/matthew-778-ask-andreligious-wall-decal-quotes-p-246.html

Safisha Roho yako na si mwili wako

Mpendwa,

Ili kuweza kumpokea Yesu wakati wa Pasaka ni vema kuanza kujisafisha Roho zetu, mambo ya nje yanayoleta sifa ya mwili au kwa wengine hayatusaidii kumpa Mungu sifa na kubarikiwa Naye, kinachoatakiwa ni kuacha maovu, huko niko kujisafisha rohoni. Yesu “ Alipokuwa akinena, Farisayo mmoja alimwita aje kwake ale chakula; akaingia, akaketi chakulani. Farisayo huyo alipomwona, alistaajabu kwa sababu hakunawa kabla ya chakula. Bwana akamwambia, Ninyi Mafarisayo mwasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani yenu mmejaa unyang’anyi na uovuEnyi wapumbavu; aliyevifanya vya nje, siye yeye aliyevifanya vya ndani pia? Lakini, toeni sadaka vile vya ndani, na tazama, vyote huwa safi kwenu. Lakini, ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili.” Luka 11:37-47

Mungu mwema nisaidie kutenda mema ili kusafisha roho yangu. Amina

Iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma

Mpendwa,

Bwana Yesu leoa anatuambia  “Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa.  Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.  Akawaambia mithali, Je! Aliye kipofu aweza kuongoza kipofu? Hawatatumbukia shimoni wote wawili?  Mwanafunzi hawi mkuu kuliko mwalimu wake, lakini kila mtu ambaye amehitimu hulingana na mwalimu wake.” Luka 6:36-40

courtesy: http://www.bible-lists.pw/Mercy/Mercy.shtml

Zishike Amri

Mpednwa,

Mungu leo anatukumbusha kuishi maisha yaliyo safi, na kuzidi kumrudia yeye. Tukiwa katika kipindi hiki cha Kwaresma cha kujuta dhambi zetu na kujisafihsa, tukingojea ufufuka wa Bwana Yesu, neno linatukumbusha kuacha mabaya tunayoyaona katika jamii kila siku na tunachotakiwa kufanya ni kutenda yale wenzatu wanayoyahitaji. Neno linatukumbusha “Msiibe, wala msidanganye, wala msiambiane uongo. Msiape uongo kwa jina langu, hata ukalinajisi jina la Mungu wako; Mimi ndimi Bwana. 

Usimdhulumu jirani yako, wala kumnyang’anya mali yake; ijara yake aliyeajiriwa isikae kwako usiku kucha hata asubuhi. Usimlaani kiziwi, wala usitie kwazo mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako; Mimi ndimi Bwana. 

Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki. Usiende huko na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usisimame kinyume cha damu ya jirani yako; mimi ndimi Bwana. 

Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, wala usichukue dhambi kwa ajili yake. Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana” Walawi 19:11-18

Basi mpondwa tumuombe sana Mungu atupe nguvu kuzishika amri zake. Amina

Saumu Niliyoichagua, ni hii

Mpendwa,

Tupo katika mwezi wa Kwaresma, siku za kujitafakari maisha yetu na kuangalia ni vipi tunakwenda sambamba na sharia za Mungu, ni wakati wa kuomba neema za Mungu ili kufanya mabadiliko katika maisha yetu na kuwa watu wema , kuacha uovu na dhambi za kila aina.

Moja ya mambo tunayoweza kufanya ili kumrudia Mungu ni kufunga, lakini je unafunga namna gani? Mungu leo anatufunulia namna bora ya kufunga, saumu ama funga aliyoichagu Mungu ni ipi? Neno linatumabia “Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana?

Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila niraJe! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?   Isaya 51:6-7

Mpendwa , hayo ndo tunaopaswa kufanya wakati wa kipindi cha Kwaresma na hata baada ya kipindi hiki. Ukibadili maisha yako na kuendana na mwongozo huo wa Mungu Baba “Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde. Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa.” Isaya 51:8

Basi Mpendwa, fanya funga iliyo bora, upate baraka za Mungu.

Tuombe:

Mungu Baba wa Mbinguni, asante kwa kunipa uzima na kuufikia wakati huu wa kujitafakari na kukurudia wewe, nipe neema zako niweze kufunga kwa kuwajali wingine. Amina