Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? Ee Mungu, nadhiri zako zi juu yangu; Nitakutolea dhabihu za kushukuru. Maana umeniponya nafsi yangu na mauti; Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke? Ili nienende mbele za Mungu Katika nuru ya walio hai.

Zaburi 56:11-13

“Ni nani niliye naye mbinguni, Wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe.
Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele.
Maana wajitengao nawe watapotea; Umewaangamiza wote waliokuacha Wewe.
Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu; Nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU, Niyahubiri matendo yako yote.”

Zaburi 73:25-28

Je Unafikri kabla ya maamuzi?

“Wakashuka watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka. Basi baada ya Paulo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhojiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemu kwa mitume na wazee kwa habari ya swali hilo. Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulifikiri neno hilo.” Matendo 15: 1, 2, 6.

Mitume walipopata changamoto ya mafundisho ya kuwa watakaookolewa ni wale tu waliotahiriwa, na baada ya mabishano, walichofanya mitume ni kukusanyika pamoja ili “…wapate kulifikiri neno hilo”. Hapa inaonyesha kuwa mitume walitaka kupata nafasi ya kutafakari neno hilo kabla ya kutoa maamuzi, na walimwomba Mungu Roho Mtakatifu kungoza maamuzi yao. “Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia…Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi; Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua” Matendo 15: 7,8,10

Je mpendwa unapopata wakati mgumu wa kufanya maamuzi, unakaa na kufikiri juu ya jambo hilo, ama unatoa maamuzi haraka hataka? Unapaswa kujihoji sana na pia kusikiliza hoja za wengine kabla ya kufanya maamuzi, mitume walipeana hoja nyingi sana, kabla ya Petro Mtume kueleza maamuzi. Leo neno linatukumbusha tuwe watu wa kufikiri na kuomba Roho Mtakatifu kutuangazia katika kila jambo ambalo tunataka kufanya maamuzi “Kwa kuwa Bwana huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;” Mithali 2:6

Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi

Mpendwa,

Tawi ka mti, mfano wa mwembe, linapokatwa na kutupwa mbali, hata ikiwa mbali kiasi gani, unapoliona, utatambua mara moja kuwa hilo ni tawi la mti wa mwembe, inakuwa ni rahisi kutambua tawi hilo kwa sababau, LINAFANANA na mti wa mwembe. Yesu leo anatumabia “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.” Yohana 15:5. Je wewe ni tawi la mzabibu? ili kuwa tawi linalozaa, unapaswa kufanana na mti wenyewe, mzabibu, Unapaswa kufanana na Yesu, maana yake kufanya yale Yesu anayofanya, kuwa mtu wa sala, maombi, kuponya wagonjwa, kuhubiri neno la Mungu, nk, hayo ndiyo matunda ambayo Yesu anasema matawi Yake yazae. Usipofanana na Yesu unakuwa haumo ndani Yake, usipokuwa ndani ya Yesu maana yake hatufanani Naye na hauzai matunda na hivyo kama matawi yasiyozaa UTAONDOLEWA, kama Yesu mwenyewe anavyosisitiza “Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.” Yohana 15: 1-2

Basi tumwombe Mungu , kwa maongozi ya Roho  Mtakatifu , tuweze kuzaa matunda , ili tusiondolewe katika mzabibu wa kweli, tusitenganishwe na Yesu.

Mimi namtumaini Bwana

Ee Bwana,

Ndiwe genge langu na ngome yangu; Kwa ajili ya jina lako uniongoze, unichunge. Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri, Maana Wewe ndiwe ngome yangu.Nawachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo; Bali mimi namtumaini Bwana. Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako, Kwa kuwa umeyaona mateso yangu. Umeijua nafsi yangu taabuni,Ee Bwana, nisiaibishwe, maana nimekuita; Waaibishwe wasio haki, wanyamaze kuzimuni.Bwana ahimidiwe; kwa maana amenitendea Fadhili za ajabu katika mji wenye boma.

Zaburi 31:3-4, 6-8, 17, 21

Jikane ili kunfuta Yesu

Ili kunfuta Yesu , unahitaji kuachna na starehe za dunia

Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.  Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.  Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?”

Matayo 16:25-26

ourtesy:lds.org