Ndiwe sitara yangu na ngao yangu, Neno lako nimelingojea.
Enyi watenda mabaya, ondokeni kwangu, Niyashike maagizo ya Mungu wangu.

Zaburi 119:114-115

Jipe moyo Mungu yupo pamoja nawe

Mpendwa jipe moyo Mungu yupo pamoja nawe, Mungu wetu ni wa wakati wote wala hachoki, kama unaenenda katika wakati mgumu, nikupe neno la faraja ndugu, kuwa usichoke kumlilia Mungu kila siku, Sali, jiombee wewe mwenyewe Mungu akupe nguvu ya kupata mbinu za kuvuka pale ulipokwama na vile vile uwaombee wale wanaoleta makwazo juu yako, ili wabadilike. Kumbuka siku zote Mungu akausikia “Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki. Huwapa nguvu wazimiao, umwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.” Isaya 40:-28-31

Basi mpendwa Mungu na akupe nguvu.

Enenda katika Bwana Yesu

“Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana. Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu. Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;  kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.  Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana.  Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.  Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.  Katika habari ya upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.  Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia yote. Lakini twawasihi, ndugu, mzidi sana.  Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza;  ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote.”

 1 Wathesalonike 4:1-12

Msiwaogope; mkumbukeni Bwana, aliye mkuu mwenye kuogofya

Mpendwa, Amani ya Bwana na iwe juu yako.

Katika maisha ili uweze kufanikiwa kwa jambo lolote, kati ya mengi,  kuna mambo mawili ya kuzingatia, kwanza Kumkumbuka Mungu wako kuwa ananakupa nguvu na kukusaidia katika lile unalofanya, na pili kujua unafanya jambo hilo kwa lengo gani, kwa namna hiyo utapata ujasili na hutaogopa kusonga mbele katika unalolifanya , Nehemia aliwatia moyo watu wake pale maadui walipokuwa wakuja kuwavamia ansema “Nikatazama, nikaondoka, nikawaambia wakuu, na mashehe, na watu wengine waliobaki, Msiwaogope; mkumbukeni Bwana, aliye mkuu mwenye kuogofya, mkawapiganie ndugu zenu, na wana wenu, na binti zenu, na wake zenu, na nyumba zenu. Kisha ikawa, adui zetu waliposikia ya kuwa tumekwisha kupata habari, na ya kuwa Mungu amelibatilisha shauri lao, ndipo sisi sote tukarudi ukutani, kila mtu kwa kazi yake. “ Nehemeia 6:14-15

Basi mpendwa, kama walivyoambia hawa “mkumbukeni Bwana, aliye mkuu mwenye kuogofya..” na “…mkawapiganie ndugu zenu…” nawe basi mkumbuke Mungu na ukalipiganie lile lengo ulilonalo. Mungu akubariki sana.

Ukisika sauti ya Mungu , atakubariki

Mpendwa,

Unapoisika sauti ya Mungu, na kuyashika mafundisho yake , Mungu atakubariki na kukulinda, sauti ya Mungu ipo ndani ya neno lake, soma neno la Mungu, tafakari, nawe utaisika sauti, na kisha ifuate. na ” Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.  Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako”

Kumb: 28:1-8

Mtu akinipenda, atalishika neno langu

Mpendwa,

Pengine unashidwa kufanikiwa katika mambo mengi unayofanya kwa sababu Mungu hafanyi makao ndani yako, hatuna urafiki na Mungu, na ii inatokana  kutoshika neno lake. Yesu anatupenda sana na kila mara anatuambia cha kufanya ili aweze kukaa nasi “Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.” Yohana 14:23

Basi Mpendwa, soma, sikiliza, na shika neno la Mungu, naye atakuwa ndani mwako, kukuongoza na kukufanikisha kwa kila jambo.