Mpendwa

“Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;  tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.”

Waefeso 4:31-32

Ukitaka kusamehewa , Samehe Kwanza

Mpendwa,

Wanafunzi walipomwambia Yesu  wafundishe kusali, aliwafundisha , na katika sala hiyo Yeu alisisitiza sana Msamaha, Basi leo kumbuka kusamehe ni kujiponya. Na sharti kubwa ka kusamehewa ni kusamehe. Yesu anatuambia , msalipo semeni

“Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.] Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.” Matayo  6:9-15

Basi Mpendwa amua leo kusamehe , ili usamehewe, hakuna aliye mkamilifu isipokuwa Mungu tu. Omba neema ya Mungu, kwani bila neema huwezi kutoa msamaha wa kweli.

Unaamini?

Mpendwa,

Unapoamini ndipo unapofanikiwa mambo yako katika ulimwengu huu, lakini je unaamini nini au nani?  hilo ndilo kubwa , basi ili uweze kufanikiwa kiroho na kimwili Amini ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu “ Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? “ 1 Yohana 5:5.

Mungu na akubariki sana.

Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba

Mpendwa,

Kila mmoja wetu kama ilvyokuwa kwa Daniel anaweza akawa katika tundu la simba, ni nini tundu lako  la Simba?  Je ni ungonjwa ulionao, haki uliyodhulumiwa kazini, matatizo katika ndoa yako, dhuluma ya haki yako kazini?  kumbuka, kama vile Mungu alivyomtuma malaika akafunga vinywa vya simba wasimdhuru Daniel , ndugu yangu kuwa na faraja kwa kuwa Mungu wetu ni Mungu aliye hai , huponya na kuokoa,  anaona masumbuko yako, Mwombe leo naye atatuma malaika wake aje akuokoe kutoka katika tundu hilo la masumbuko yako.

Bwna na awe nawe , akuokoe na akupe furaha katika shida zako.

Daniel 6:16, 18, 21 ,25-27

Tazama, nitatenda neno jipya

Mpendwa,

Mungu anasema “Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani. “ Isaya 43:19, hebu jitafakari leo na uone ni lipi jipya Mungu amelitenda kwako, inaweza ikawa kila siku tunaomba bila kufikiri vema, kumbe kuna mengi ambayo Mungu ameyatenda kwetu, kukaa kimya na kutafakari ni vizuri ili kujua ni mema mangapi Mungu amekutendea. Barikiwa Sana leo

Bwana yu Mwema

Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote; Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba; Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake. Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake; Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi.

Zaburi 100

Sikia maneno ya Nabii ni maneno ya Mungu

“Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake. Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza ulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa.”

Kumb 18: 18-20