Omba na fanya kazi kwa bidii

Kwani

Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji.”

Mithali 21:5

Unyenyekevu ni huduma

Mpendwa,

Unyeyekevu si unyonge wala kudharaulika, bali ni huduma, na kwa kuwa mnyenhyekevu, si kwamba watu tu wanaokupa heshima bali hata Mungu anakupa nafasi katika ufalme wake. Unapaswa kuwa mnyeyekevu katika kuwahudumia wengine, kama wewe ni baba je, unajinyeyekeza namna gani kuihudumia familia yako, kama ni mama wewe unajinyeyekeza namna gani kuona familia ipo katika hali nzuri, na kama ni mtoto unajinyenyekeza vipi kuwaheshimu na kuwatii wazazi na wakubwa. Tunapokuwa katika mahali pa kazi na sala ni vema tukajinyeyekeza katika kuwahudumia wengine, kwani ukijishusha ndipo Mungu atakuweka mahali pa juu. Yesu anatuambia mfano huu “Akawaambia mfano wale walioalikwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya mbele; akisema, Ukialikwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe, akaja yule aliyewaalika wewe na yeye, na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma. Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe. Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.

Luka 14:7-11

Ubarikiwe

Je, upo tayari?

Mpendwa,

Mungu anapenda tujiweke tayari kila mara, kuwa tayari au kukesha ni kuwa watu wa matendo mema na kuacha dhambi za aina zote, ili ajapo atukute tunakesha ” Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.” Matayo 24:42:44

Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu. Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.

1 Wathesalonike 4:2-5

Hakuna atakayetutenga na upendo wa Kristo

Mpendwa,

Mungu natupenda sana na ndiyo maana alimtuma Mwanye , Bwana Yesu atukomboe na kutuaondolea dhambi zetu, ni upendo wa hali ya juu. Yesu alitupenda na anaendela kutupenda daima, na hakuna kitu chochote kjinach0weza kututenga na upendo huo. Waweza ukawa katika hali ambayo unaweza ukafikiri umetengwa na upendo wa Yesu lakini sivyo,  neno linasema ”  Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?  Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.  Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.  Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,  wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote HAKITAWEZA kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu

Warumi 8:35-39

Mpendwa,

Mungu Baba anajua kila kitu hata mawazo yetu na mipango yetu hivyo utapaswa kuwa na imani na kila jambo linalotokea katika maisha, kwani katika neno lake anatumabia “ Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. ” Yeremia 20:11

Barikiwa sana.