Kuwa na mali si dhambi

Mpendwa,

Mungu anatupa nafasi ya kujitafutia riziki na kuwa na mali, si jambo baya kuwa na mali nyingi, lakini je unazipataje na unazitumiaje?. Mara nyingi tunakuwa watu wa kujiwazia sisi wenyewe na familia zetu, utaona Mpendwa mmoja anasema mali hii ni kwa ajili ya wanangu, ni kweli ni vema tukaweka akiba kwa ajili ya watoto na jamaa zetu, lakini je kama kuna Mpendwa mwingine jirani ana shida kubwa ya ugonjwa au hana chakula, utaacha kumsaidia tu kwa sababu unaweka akiba ya watoto? Huo ni ubinafsi. Mungu leo anatuasa tusiwe watu wa choyo, “Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.” Luka 12:15. Tusiweke akiba ya nafsi zetu bali tujitajirishe kwa Mungu. “Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.” Luka 12:20, Na kujitajirisha kwa Mungu, ni kwa kuwakumbuka wengine kwa mali tulizojaliwa na Mungu.

“Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu.  Akamwambia, Mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu?  Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo. Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;  akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.  Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.  Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.  Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?  Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.”  Luka 12:13-21

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s