Leo Yatosha…One Day at a time

“Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake ” Matayo 6:34

Courtesy: YouTube

Onyesha Kipaji chako

Kama una jambo lililo moyoni na lina faida kwa wengine, iwe ni la kidunia au la Kimungu, usilifiche ndani ya Moyo wako, liweke hadharani, lifundishe, kwa ajili ya faida ya wengine kama ilivyo mwaka wa Taa;  kwani Yesu anasema “Hakuna mtu awashaye taa na kuiweka mahali palipositirika, au chini ya pishi; bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuuona mwanga.” Luka 11:33

Kwanini Sala au Maombi yako hayajibiwi

Mpendwa,

Umekuwa ukiomba kwa Mungu mara nyingi sana, lakini pengine huoni matunda ya sala na maombi yako, ni kwa nini?. Je, umejichunguza?, wakati mwingine unaomba ukiwa bado hujajipatanisha na Mungu, dhambi zimekuzunguka, je Mungu anasikia sala ya Mwenye dhambi? la hasha, neno lasema “Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu. Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya; ” Isaya 1:15-16, Mungu anataka tuwe safi tunapomwomba na ndipo hataficha macho yake, unapotubu dhambi unaunganika na Mungu, naye anakujalia unayoyaomba. Basi mpendwa tubu, na Mungu atasikia sala yako ukimwomba.

Barikiwa sana

Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao

Mpendwa,

Mungu akubariki. Leo Mungu anapenda umtolee kupitia wahitaji. Kuna wakati unakuwa hauna sababu maalumu ya kutotoa, lakini Mungu wetu ni mwema haachi kutukumbusha kutenda mema ili tuweze kubarikiwa. Neno linasema “Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda. Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; Nawe unacho kitu kile karibu nawe. ” Mithali 3:27-28; Sasa je unafanya nini kusaidia wahitaji wakati unao uwezo wa kufanya hivyo, usiwe na kisingizio cha kutompa mhitaji, kumbuka unapo mpa mhitaji huyo, unampa Mungu mwenyewe Naye atakujaza baraka, kwani “Wenye hekima wataurithi utukufu, Bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha.” Mithali 3:35. Basi kuwa mwenye hekima kwa kutenda mema nawe utaurithi utukufu.

Ondoka sasa ,angali mhitaji aliyekaribu nawe na mpe kile unachodhani kinafaa kwa ajili yake.

Barikiwa Sana