Kwanini kuomba wakati Mungu anajua?

Mpendwa,

Ulishawahi kujiuliza kwa nini unaomba wakati Mungu anajua hata kabla hujaomba? Neno linasema “Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.” Isaya 65:24, tena Yesu mwenyewe anasema “Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.” Matayo 6:8

Kwanza napenda kukupa moyo usiache kuomba kwani Baba Mungu Mwenyezi ameshakuhakikishia kuwa anajua na kuyajibu maombi yako, siku zote dumu katika sala na kuomba. Mungu anataka uombe ingawa anajua unachotaka kwani anataka kuona unyeyekevu wako “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake” 1 Petro 5:6, anapenda asikie ukitamka mwenyeywe matakwa yako kutoka katika kinywa chako, hivyo Mpendwa kuwa mnyeyekevu na enenda mbele zake na kusema bila woga mahitaji yako yote, naye kwa kuwa ameshayajua unayohitaji atakupatia.

Ubarikiwe na Bwana

Hope
Courtesy: http://greatergood.berkeley.edu/

Usichike Kungoja…

Mpendwa,

Usishahau “… neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba” 2 Petro 3:8-9, hivyo basi lolote unaolomwomba  Mungu, kumbuka lipo katika kapu lake na hajasau , atakupa kwa wakati wake.

Ubarikiwe

Kufuata Sheria ni Kufanikiwa

Heri ni neno linalomaanisha, uzuri au jambo jema; Mpendwa unapofuata sheria (za Mungu na za Wanadamu) unapata heri yaani unapata baraka toka kwa Mungu na mambo yako yanakwenda vizuri, ndiyo maana mzaburi anasema “ Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya Bwana.  Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote.” Zaburi 119:1-2, basi fanya bidii kuzifuata njia za Bwana. Ili kupata heri unapaswa kufanya bidiii kuacha dhambi na kufundishwa na Bwana “ Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. Ee Bwana, umehimidiwa, Unifundishe amri zako.” Zaburi 119:11-12. Fanya bidii huku ukiomba Mungu akutendee mema , akupe nguvu kulitii neno lake ambalo ndiyo sheria yenyewe “Umtendee mtumishi wako ukarimu, Nipate kuishi, nami nitalitii neno lako.  Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako. “ Zaburi 119:17-8.

 Ubarikiwe