Mungu huwasikiliza Wacha Mungu

Mpendwa,

Unajitafakari vipi katika maisha yako, umeshawahi kumwomba Mungu lakini hupati unachoomba? ulishafikiri ni kwanini; pengine unaweza firiki Mungu hakupendi ama  hayupo nawe, lakini ukweli Mungu nakupenda sana, isipokuwa hali ya Roho yako ndiyo inayomhuzunisha Mungu na kutosikiliza maombi yako. Neno linasema “Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.” Yohana 9: 31. Basi Mpendwa acha dhambi, na ishi kwa kumcha Mungu na kutenda mema, hapo ndipo Mungu atasikia maombi yako

I Surrender – Ukae Kimpya Mbele Za Bwana

Ukae kimya mbele za Bwana, Nawe umngojee kwa saburi; Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu afanyaye hila. Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya. Maana watenda mabaya wataharibiwa, Bali wamngojao Bwana ndio watakaoirithi nchi.

Zaburi 31:7-9

Courtesy: YouTube

Bwana Nisamehe

Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.

Zaburi 51:1-4

Courtesy: YouTube

Mpe Bwanas Sifa

Njoni, tumwimbie Bwana, Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu. Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi. Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba. Kwa maana ndiye Mungu wetu, Na sisi tu watu wa malisho yake, Na kondoo za mkono wake. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! Msifanye migumu mioyo yenu; Kama vile huko Meriba Kama siku ya Masa jangwani. Hapo waliponijaribu baba zenu, Wakanipima, wakayaona matendo yangu.

Zaburi 98:1-2,6-9

Toa Matunda kwa wakati wake

Mungu ametuweka hapa duniani, ili tuitunze  dunia hii na kutoa matunda mema yaani matendo yetu, je tunazaa matunda, tunatoa mazao yanayohitajika. Mungu anatuma watumishi wake kutueleza namna na kuzaa matunda na kututaka kutoa hayo matunda/mazao kwake Mungu, je tunawasikiliza watumishi hawa au tunakuwa kama wale wakulima waliopangishwa na walitakiwa kutoa matunda,  lakini badala yake waliwapiga na waliwaua watumishi waliotumwa kuchukua matunda? Hata ikafikia hatua wakamwuua Mwana wa mwenye shamba ili warithi lile shamba wao. Leo Mungu anatutaka tuzae matunda mema na tumpokee Yesu anayekuja  kutukomboa sisi sote la sivyo hukumu kubwa itatupata. Tubu kwa maana ufalme wa Mungu umekaribia.

Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake. Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe. Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza wakawatenda vile vile. Mwishowe akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu. Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake. Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. Basi atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawatendaje wale wakulima? Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake. Matayo 22:33-41

Mtegemee Mungu utabarikiwa

Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.

Yeremia 17:7-8

Courtesy: YouTube