Twaeni, mle, huu ndio mwili wangu

Walipokuwa wanakula, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema, ‘‘Twaeni, mle, huu ndio mwili wangu.’’ Kisha akachukua kikombe, akashukuru, akawapa akisema, ‘‘Kunyweni nyote katika kikombe hiki. Hii ndiyo damu yangu ya agano, ile imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. Lakini ninawaambia, tangu sasa sitakunywa tena kutoka katika uzao huu wa mzabibu, mpaka siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika Ufalme wa Baba yangu.’’ Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka kwenda mlima wa Mizeituni Matayo 26: 26-30

Bwana akubarikie, na kukulinda;
Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili;
Bwana akuinulie uso wake, na kukupa amani.
Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabarikia.

Hesabu 6:24-26

Amri Kuu

Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.  Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.

Matayo 22:36-40