Unapoitwa, Itika

Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani, aitwaye Mathayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata.Ikawa alipoketi nyumbani ale chakula, tazama, watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja wakaketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake. Mafarisayo walipoona, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi. Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.

Matayo 9:9-13

Mishirikihe mungu katika kila jambo

Mpendwa,

Upendo wa Kristo na uwe juu yako.

Napenda kukushirikisha jambo moja leo. Kila unapofanya jambo ni muhimu sana kumshirikisha Mungu,  neno linasema ” Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye:  Wakolosai 3:17. Mungu pekee anaweza kukuongoza na kufanikiwa katika jambo unalofanya , kwani unaposhirikisha Mungu unakuwa upo ndani Yake, na neno linatukumbusha “…akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana..” Yohana 15:5 , hivyo ili ukitaka kuzaa zaini yaani kufanikiwa na kusonga mbele kiroho na kimwili ni vema kutumaini na kumpa mambo yako Mungu ” Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.”  Mithali 3:-5-6

Upendo ni nini?

“…Mungu ni upendo,  …Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. …Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;  haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;  haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.”

1 Yoh 4:8,  1 Yoh 3:16,, 1 Kor 3:4-8

Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha.
Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.
Usikubali mashitaka juu ya mzee, ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu.
Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope.
Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.
Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi.

1 timother 5:17-22