Mtu asiye haki

Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia, Una nini wewe kuitangaza sheria yangu, Na kuliweka agano langu kinywani mwako? Maana wewe umechukia maonyo, Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako. Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye, Ukashirikiana na wazinzi. Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, Na ulimi wako watunga hila. Umekaa na kumsengenya ndugu yako, Na mwana wa mama yako umemsingizia. Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza; Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe. Walakini nitakukemea; Nitayapanga hayo mbele ya macho yako. Yafahamuni hayo, Ninyi mnaomsahau Mungu, Nisije nikawararueni, Asipatikane mwenye kuwaponya. Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.

Zaburi 50:16-23

Our Father..forgive us our trespasses

Our Father, Who art in heaven
Hallowed be Thy Name;
Thy kingdom come,
Thy will be done,
on earth as it is in heaven.
Give us this day our daily bread,
and forgive us our trespasses,
as we forgive those who trespass against us;
and lead us not into temptation,
but deliver us from evil. Amen.