Rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu

Mpendwa,

Tunaanza kipindi cha Kwaresma, ni kipindi cha kufanya mabadiliko, kufanya upya maisha yetu, kukumbushana kuhusu kutubu, kusali na kutenda mema zaidi.  Ni wakati wa kufunga na kujinyima yale mazuri tuyapendayo, na kwa kujima huko tuwasaidie wale wasiokuwa nacho, na ni wakati wa kuomba zaidi. Ni wakati wa kubadilika na kuacha dhambi “ Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea;  rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya.” Yoeli 2:12-13.

Basi mpendwa, tumwombe sana Mungu mwema, katika siku hizi arobaini, tunapongojea ufufuko wa Bwana Wetu Yesu Kristo, tufanye yote yaliyo mema, na baada ya kumaliza mfungo huu, tuendeleze yale yote tuliyoyavuna katika kipindi hiki cha Kwaresma.

Mungu Akubariki.

Courtesy: https://www.catholiccompany.com/getfed/ash-wednesday-beginning-lent/
Tubuni na Kuiamini Injili

Mtumaini Mungu Akupae vitu vyote

Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha. Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;  huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.

1 Timotheo 6:17-19