Mche Bwana, Mungu atakubariki

Mpendwa

Moyo wako usiwahusudu wenye dhambi; Bali mche Bwana mchana kutwa; 
Maana bila shaka iko thawabu; Na tumaini lako halitabatilika. 
Sikia, mwanangu, uwe na hekima, Na kuuongoza moyo wako katika njia nje

Mothali 23:17-19

Hakuna wa kukutenga na upendo wa Mungu

Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye? Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.”

Warumi 8:31-32,35,37-39

Mpendwa,

Ukichukulia katika hali ya kawaida mtu asiyekujua akajitoa kukuokoa katika tabu fulani, huo ni upendo wa juu sana. Mungu anatupenda sana , hata alipoona dunina inaangamia akamleta mwanaye Yesu kutuokao. Basi Mungu alipotuokoa alionyesha  na anaendelea kutuonyesha upendo wa juu sana,  na kwa upendo huo, ni dhahiri kwamba tukimwanini yeye , hakuna jambo lolote litakalofanya sisi tutengane na upendo huo, kwa maana kwamba hata tukipata taabu ya aina gani , tukikumbuka matendo yake makuu, hatuna haja ya kukata tamaa, kwani tunajua yupo nasi na anatupa amani kwa wakati wake. Tuombe basi Mungu atupe neema ya kukumbuka na kuamini siku zote kuwa yeye ni mwenye upendo daima.

Ukimya wa Moyoni

Ukae kimya mbele za Bwana, Nawe umngojee kwa saburi; Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu afanyaye hila.  Zaburi 37:7

Mpendwa,

Leo napenda tutafakali pamoja kuhusu ukimya. Mara nyingi , tumekua tukifanya sala binafsi au za pamoja , tumekuwa tukitoa sifa na shukrani kwa  Bwana Mungu kwa wema wake, na hilo ni jambo jema sana. Lakini je ni mara ngapi tumepata muda wa kuwa kimya bila kuomba , kusifu au kutoa shukrani, kukaa kimya tukimsililiza Bwana Mungu anataka nini kwetu. Je unapata muda wa kuwa kimya, akilini na moyoni mwetu ukimgojea Bwana kusema neno nawe, ukimya ni jambo jema ili kumsililiza Mungu anasemaje, kuna wakati unatakiwa kujua Mungu anataka ufanye nini juu ya ulimwengu huu, na ni kwa kukaa kimya na kumsikiliza ndipo utajua nini Mungu anachotaka kwako. Basi tumwombe Bwana atujalie tuwe na nafasi ya kukaa kimya kimwili na kiroho ili atujulishe mengi kwa ajili ya kumtukuza katika ulimwengu huu.

je huwa unajitengea muda wa ukimya na tafakari au umewahi kupata muda wa ukimya na tafakali?