Rafiki hupenda sikuzote…

Mithali 17:17

Upendo

Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote

1 Kor 13:4-7

Sala ya kuoomba Nguvu ya kusameha

Bwana Mungu, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe. Ninakuomba Ewe Mungu, niondolee moyo wa woga; maana Wewe u pamoja nami; ulisema Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.  Mungu Mwema Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu, na kuliachilia kosa la watu wa urithi wake waliosalia? Nipe moyo wa kusamahe.

Mungu Baba ulisema nisipowasamehe wenigne  , Mungu Baba hutanisamehe, Bwana Mungu nipe moyo wa kusamehe, niondeolee uchungu ndani ya moyo wangu, Wewe unanihurumia; utayakanyaga maovu yangu; nawe utazitupa dhambi zangu zote katika vilindi vya bahari. Yaondoe mchungu yangu ukayatupe kwenye Bahari yasinirudie tena, nipe moyo wa kusamehe.

Wewe Bwana Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo, Bwana Mungu, moyo wangu umezimia, nafsi yangu imeyeyuka kwa uzito, Unitie nguvu sawasawa na neno lako. Ninajua Bwana Nayaweza mambo yote katika wewe unitiaye nguvu. Nipe Nguvu za kusamehe.

Bwana nakuongojea wewe sasa unipe nguvu ya kusamehe , kwani ulisema “wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.” Nipe nguvu za kusamehe.

Ninakuomba sasa nipige mbio na kwenda kusamehe kwa moyo mkuu. Nipande juu kama tai na ninaachilia uchungu wote na ninakuwa huru sasa. Ninaomba neema Mungu Baba, nitie baraka na sasa naamua kusamehe, Asante Mungu, kwani wewe unaniweka huru. Ninaomba na kushuku kwako Mungu wa milele. Amina.

Zaburi 119:28; 130:3-4, Isaya 40:29,31; 43:25, 55:7, Mika 7:18-19, Wafilipi 4:13

Samehe nyakati zote, mara zote

Mpendwa, 

Kuna wakati mtu wanakukosea mara kwa mara mpaka basi, inafikia wakati unashindwa cha kufanya , kwani unakuwa umesamehe mtu mara nyiiingi lakini anarudia kosa lilelie. Leo Mungu anatuambia tusichoke katika kusamehe “Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe. Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe. ” Luka 17:3-4. Basi omba sana Mungu akupe moyo wa kuendelea kusamehe katika hali zote na katika nyakati zote. 

Kila Msamaha una malipo

Mpendwa,

Ukisamehe Mungu naye analipa hicho ulichokifanya, na usiposamahe ni hivyo hivyo, basi jiweke huru upate zawadi ya msamaha kwa kusamehe. Yesu anatuambia ” Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. ” Matayo 6:14-15, Samehe upate malipo ya msamaha.