Mungu tu, hufungua siri zote

Mpendwa,

Nakusalimu kwa jina la Bwana .

Siku zote katika maisha unapokuwa na jambo ambalo hujui suluhisho lake, mwendee Mungu naye atakufanya kujua suluhisho lake, yeye ndiye ajuaye siri ya kila fumbo hapa duniani, usimweleze mwanadamu siri zako, kwani mwanadamu si kitu na hawezi kufumbua siri za matatizo au maswala yanayotusibu.  Mkumbuke mfalme Nebukadreza, nsoto yake haikuweza kutafiriwa na watu, bali Daniel ambaye aliomba hekima ya mungu kujua ndoto na tafsiri yake. Ndipo Danielii akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake; ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo, ili kwamba Danielii na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli. Ndipo Danielii alipofunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku. Basi Danielii akamhimidi Mungu wa mbinguni.” Daniel 2:17-19,

Ongoza watu katika kutenda haki, utang’aa milele

Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele. Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele. 

Daniel  12:1-3

Mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu

Mpendwa,

Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.  Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.  Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;  maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

1 Kor 6:16-20

Atendaye haki yuna haki,

Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake

1 Yohane 3:7-10