Ombeni kwa jina Langu

Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.

Yohana 16:23-24

NITAFUNGAJE MWEZI HUU WA KWARESMA?

 • Acha kuongea maneno ya kuumiza, ongea wema kwa wengine
 • Acha huzuni , kuwa na moyo wa shukrani
 • Acha Hasira , kuwa mvumilivu
 • Acha tamaa, kuwa na matumanini
 • Usiwe mwoga , Mwamini Mungu
 • Acha kulalamika, kuwa na unyenyekevu
 • Acha kuwa na wasiwasi, kuwa mtu wa sala
 • Ondoa uchungu, jaza furaha moyoni mwako
 • Acha ubinafsi kuwa na huruma kwa wengine
 • Sahau ya zamani , samehe waliokukosea
 • Zungumza kidogo, Sikiliza Zaidi.

 Maneno ya papa Fransisko
Courtesy: tafsiri isiyo rasmi -whatsapp

Unazaa Matunda?

Mpendwa,

Je maisha yako ni kama mzabibu unaozaa matunda, je wewe ni mfano wa maisha ya Kimungu au wewe ni kikwazo, Mungu anatoa nafasi ili kujiweza safi kiroho, unajipangaje, usipozaa matunda, usipoishi maisha ambayo yanampendeza Mungu na wanadamu , basi utakatwa kama mzabibu usiozaa. “ Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate. Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu? Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate.”  Luka 13:7-9

Basi ninyi salini hivi;

Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe,Ufalme wako uje, 
Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. 
Utupe leo riziki yetu. 
Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. 
Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.] 

Matayo 6:9-13