Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu

Ee Mungu, moyo wangu u thabiti, Nitaimba, nitaimba zaburi, Naam, kwa utukufu wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri. Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu, Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa. Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni, Na uaminifu wako hata mawinguni. Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.

Zaburi 108: 1-5

Matokeo ya ukahaba

Kwa sababu hiyo, Ewe kahaba, lisikie neno la Bwana; Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu uchafu wako umemwagwa, na uchi wako umefunuliwa, kwa njia ya uzinzi wako pamoja na wapenzi wako; na kwa sababu ya vinyago vyote vya machukizo yako; na kwa sababu ya damu ya watoto wako, uliyowapa; basi, tazama, nitawakusanya wapenzi wako wote ambao umejifurahisha pamoja nao, nao wote uliowapenda, pamoja na watu wote uliowachukia; naam, nitawakusanya juu yako pande zote, na kuwafunulia uchi wako, wapate kuuona uchi wako wote. Nami nitakuhukumu, kama wahukumiwavyo wake walioolewa wazinio, na kumwaga damu, nami nitakupatiliza damu ya ghadhabu na wivu. Tena nitakutia katika mikono yao, nao watapaangusha mahali pako pakuu, na kupabomoa mahali pako palipoinuka, nao watakuvua nguo zako, na kutwaa vyombo vyako vya uzuri, nao watakuacha uchi, huna nguo.  Tena wataleta mkutano wa watu juu yako, nao watakupiga kwa mawe, na kukuchoma kwa panga zaoNao watazipiga moto nyumba zako, na kutekeleza hukumu juu yako mbele ya wanawake wengi, nami nitakulazimisha kuacha mambo ya kikahaba, wala hutatoa ujira tena.  Hivyo ndivyo nitakavyoshibisha ghadhabu yangu juu yako, na wivu wangu utanitoka, nami nitatulia wala sitaona hasira tena.  Kwa sababu hukuzikumbuka siku za ujana wako, bali umenikasirisha kwa mambo hayo yote; basi, tazama, mimi nami nitaleta njia yako juu ya kichwa chako, asema Bwana MUNGU; wala hutafanya uasherati zaidi ya machukizo yako yote.

Mtumaini Bwana Daima

Haleluya. Ee nafsi yangu, umsifu Bwana.  Nitamsifu Bwana muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.  Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.  Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.  Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, Na tumaini lake ni kwa Bwana, Mungu wake,  Aliyezifanya mbingu na nchi, Bahari na vitu vyote vilivyomo. Huishika kweli milele,  Huwafanyia hukumu walioonewa, Huwapa wenye njaa chakula; Bwana hufungua waliofungwa;  Bwana huwafumbua macho waliopofuka; Bwana huwainua walioinama; Bwana huwapenda wenye haki;  Bwana huwahifadhi wageni; Huwategemeza yatima na mjane; Bali njia ya wasio haki huipotosha.  Bwana atamiliki milele, Mungu wako, Ee Sayuni, kizazi hata kizazi. Haleluya.

Zaburi 146

Tips to Heal and Have Better life

  1. Good Sleep – have a good quality sleep, while we sleep inflammation automatically reduces change of heaving diseases such diabetes, cancer  and the like.
  2. Emotional health  – control your stress, do not be attached to your stress,  Find the path  where you have faith.
  3. Self Discipline – if you have to achieve anything, you must self discipline, if you have ego and pride self discipline will be difficult for you.

Courtesy: WhatApp post.

Mwaliko wa kumsifu Bwana

Njoni, tumwimbie Bwana, Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu. 
Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi. 
Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote. 
Mkononi mwake zimo bonde za dunia, Hata vilele vya milima ni vyake. 
Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya, Na mikono yake iliumba nchi kavu. 
Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba. 
Kwa maana ndiye Mungu wetu, Na sisi tu watu wa malisho yake, Na kondoo za mkono wake. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! 

Zaburi 95:1-7

Jipeni moyo, msiogope

Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi. Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa Bwana, ukuu wa Mungu wetu. Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea. Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi.

Isaya 35:1-4