Mungu Hapendi Mtu yeyote Apotee

Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je! Hawaachi wale tisa na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea? Hata akipata kumwona, amin, nawaambia, amfurahia huyo zaidi, kuliko wale tisa na tisini wasiopotea. Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee

Matayo 18:12-14

Mwimbieni Bwana, nchi yote

Mwimbieni Bwana, nchi yote; Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.
Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake.
Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana; Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
Maana miungu yote ya watu si kitu; Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu.
Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake.
Mpeni Bwana, enyi jamaa za watu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu.
Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu;
Tetemekeni mbele zake, nchi yote.
Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie; Na waseme katika mataifa, Bwana ametamalaki;

Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria

Laiti hao wanaowatia mashaka wangejikata nafsi zao! Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.  Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako. Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana.
16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.  Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.

Wagalatia 5:12-18