Maombi ya Mwadilifu

Courtesy: https://brilliantperspectives.com/crafting-a-prayer/Ee Bwana, usikie haki, ukisikilize kilio changu, Utege sikio lako kwa maombi yangu, Yasiyotoka katika midomo ya hila.  Hukumu yangu na itoke kwako, Macho yako na yatazame mambo ya adili.  Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika, Utege sikio lako ulisikie neno langu.  Dhihirisha fadhili zako za ajabu Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia; Kwa mkono wako wa kuume Uwaokoe nao wanaowaondokea.  Unilinde kama mboni ya jicho, Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako;  Wasinione wasio haki wanaonionea, Adui za roho yangu wanaonizunguka

Zaburi 17:1-2, 6-9

 

Mtapewa saa ile mtakayosema.

Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa. Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.

Matayo 10:17-20

Mungu Huwainua wadogo

Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.  Kwa sababu hiyo atawatoa, hata wakati wa kuzaa kwake aliye na utungu; ndipo hayo mabaki ya nduguze watawarudia wana wa Israeli. 

Mika 5:2-3

Watu wabaya hawaelewi na hukumu; Bali wamtafutao Bwana huelewa na yote.  Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake, Kuliko mpotofu wa njia angawa ni tajiri. Yeye aishikaye sheria ni mwana mwenye hekima; Bali aliye rafiki wa walafi humwaibisha babaye. 

Mithali 28:5-7

Jipeni moyo, msiogope

Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi. Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa Bwana, ukuu wa Mungu wetu. Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea.  Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi.

Isaya 35:1-4

Kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye

Mpendwa

Kuna wakati mtu unatenda dhambi sana, na Mungu kwa kweli huwa anahuzunika sana mtu unapotenda dhambi. Lakini Mungu ni mwema sana na anahuruma sana. Mara nying Yeye Mungu mwenyewe ndiye kukutafuta kule dhambini ulipo ili urudi  Luka 15:4 “Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone?. Na pale unapotubu na kurudi, Mungu huwa ana anafurahi. Luka 15:7 Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.

Ndugu yangu, basi zingatia moyoni kama mwana mpotevu, rudi na mwambie Mungu akusamehe, na atakupokea kwa shangwe

courtesy : https://www.pinterest.it

Haja zenu na zijulikane na Mungu

Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

Wafilipi 4:4-7

Basi, nina sababu ya kuona fahari katika Kristo Yesu mbele za Mungu.  Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yangu, Mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo, kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu; hata ikawa tangu Yerusalemu, na kando kando yake, mpaka Iliriko nimekwisha kuihubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu;  kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine; bali kama ilivyoandikwa, Wale wasiohubiriwa habari zake wataona, Na wale wasiojasikia watafahamu.

Ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu;  kwamba niokolewe na wale wasioamini katika Uyahudi, na tena huduma yangu niliyo nayo huko Yerusalemu ikubalike kwa watakatifu

Warumi 15: 18-21, 30-31