Na amani ya Mungu, itawahifadhi mioyo yenu

Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu

Wafilipi 4:6-7

Simama Imara katika Imani

Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu. Na Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu, aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema, awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema.

2 Wathesalonike 2:15-17

courtesy: Image processed by CodeCarvings Piczard ### FREE Community Edition ### on 2019-08-14 14:31:32Z | http://piczard.com | http://codecarvings.com

 

 

 

Kuwa na kiasi ni jambo jema

Kuhusu Kiasi,
Mwanangu, jijaribu nafsi yako maadamu u mzima, uviangalie vitu visivyokufaa, usijipatie hivyo. Kwa maana si vitu vyote viwafaavyo watu wote, wala siyo kila mtu apendezwaye na kila kitu. Usione uchu wa anasa yoyote, wala usiwe na choyo kwa habari ya vyakula vyako. Yaani, katika wingi wa vyakula kuna ugonjwa, na ulafi uzidio waleta msokoto wa tumbo. Wengi wamekufa kwa sababu ya kula kwa pupa, bali mwenye kujihadhari atauzidisha uzima wake.
Yoshua bin Sira 37:27-31

Hekima ni mti wa uzima

Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu. Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye. Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto. Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani.  Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye. Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara;  Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika; Na mawingu yadondoza umande.

Mithali 3:13-20