Sababu za Roho ya Kutosamahe

Kusamahe ni hali ya kufuta moyoni yale mtu aliyokukosea. Ukitafakari kwa undani zaidi yaweza ikawa sio msamaha kwa mtu pekee, bali kusamahe kila kiumbe , mnyama aliyekukosea , mazingira yaliyokukosea nk. kwa ujumla ni kuachilia na kuwa huru ndani ya moyo wako kwa makwazo uliyoyapata. Yesu anatukumbusha, Msiposamahe wengine nanyi hamtasamehewa (Matayo 6:14–15). Neno la Mungu linatutaka tuwe na roho ya kusamehe, tuwe wa kwanza kusamehe.  Kama hautasamahe ni ngumu Baba Mungu kukusamahe wewe.

KWA NINI TUNSHINDWA KUSAMAHE:
Roho ya kutosamehe husababishwa  na mambo mengi, ikiwamo

  1. Kotojua upendo wa Mungu: Kushindwa kujua na kutafakari upendo wa Mungu kwa binadamu, Mungu anatupenda sana, neno linatuambia “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16), usipojua upendo wa Mungu, utakuwa na roho ya kutosamahe.
  2. Kushindwa kukumbuka kuwa hakuna aliye mkamilifu “hakika hakuna mtu mwadilifu duniani atendaye mema daima bila kutenda dhambi” (Muhubiri 7:20). mtu ukijiona ni mkamilifu , hutaweza kusamahe.
  3. Kushidwa kujisamahe: Kutojisamehe kwa mtu binafsi, usipoanza na kujisamehe ni ngumu kusamahe wengine.

TUNAPASWA KUSAMEHE , TUFANYEJE?
Basi ni vema kujitahidi kusamahe, na ili uweze kusamahe , mtu anahitaji Neema ya Mungu , pamoja na hilo

  1. Salama na Maombi: Ni vema kusali na kuomba sana kwani kwa sala na maombi, Roho wa Mungu atatoa neema ya kusamahe na kusahau. “Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.”(1 Kor 12:8-9)
  2. Achilia Mizigo kwa Mungu: Mtu anapaswa kujisamehe na kumpa Mungu mizigo yote ili kuwa mwepesi rohoni, hii  itasaidia kuachilia msamaha… “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha”( Matayo 11:28 ) , ili uweze kusamahe “Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza …”( Zaburi 55:22
  3. Nyenyekea kwa Mungu ili ashughulikie mambo yako nawe utasamehe na kubaki na amani “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.” (1 Petro 5:7)

FAIDA YA KUSAMAHE:
Faida kubwa ya kusamahe ni kuwa: Ukisamahe Mungu naye atakusamahe, “Kama mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe na ninyi;  lakini msipowasamehe watu makosa yao, Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.” Matayo 6:14–15, kila mmoja anapenda kusamehewa na kuwekwa huru, basi samehe nawe utasamahewa. Mbali ya faida za kiroho, kimwili ukisamahe unakuwa na afya njema kwa kundoa msongo wa mawazo na magonjwa mbali mbali, kusamehe kunakufanya uweze kupata nafasi ya kufanya mambo ya maendeleo kwani hutakuwa na muda wa kumwaza mtu ambaye hutaki kumsamehe.

HITIMISHO
Kusamahe in rahisi sana kama tukiwa na upendo, mmoja wa waandashi alipomuuliza Yesu amri kuu ni ipi “Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii , Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.”  Marko 12: 29-31. Basi kama ukimpenda mwenzako hutataka kumtendela lilio baya, na hivyo akikosa utamsamahe.

TUOMBE NEEMA YA MUNGU ILI KUYAWEZA HAYA.

Reference

Three Reasons You Can’t Forgive

Verses of Hope for Struggling with Forgiveness


https://getupministry.wordpress.com/2011/05/27/10-reasons-why-forgiveness-is-so-important/
https://www.allaboutgod.com/definition-for-forgiveness-faq.htm

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.