Ukimwacha Mungu, atakukatilia mbali

Ikawa Sulemani alipokwisha kuijenga nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme, na mambo yote yaliyoingia moyoni mwake Sulemani, naye akataka kuyafanya, basi, Bwana akamtokea Sulemani mara ya pili kama alivyomtokea huko Gibeoni. Bwana akamwambia, Nimeyasikia maombi yako na dua zako, ulizotoa mbele zangu. Nimeitakasa nyumba hii uliyoijenga ili niweke jina langu humo milele; tena macho yangu na moyo wangu utakuwapo hapo siku zote; na wewe, ukienda mbele zangu kama alivyokwenda Daudi, baba yako, kwa ukamilifu wa moyo, na kwa adili, kufanya hayo yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, ndipo nitakapokifanya imara kiti cha ufalme wako juu ya Israeli milele; kama nilivyomwahidia Daudi, baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kukaa katika kiti cha enzi cha Israeli. Bali mkighairi, mkaacha kunifuata, ninyi na watoto wenu, msizishike sheria zangu na amri zangu, nilizoziweka mbele yenu, tena mkienda na kuitumikia miungu mingine na kuiabudu, basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote. Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atasituka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini Bwana ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya? Na watu watajibu, Kwa sababu walimwacha Bwana, Mungu wao, aliyewatoa baba zao katika nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine na kuiabudu na kuitumikia, basi ndiyo sababu Bwana ameleta mabaya haya yote juu yao.

1Wafalme 9:1-9

2 thoughts on “Ukimwacha Mungu, atakukatilia mbali

 1. Asante nimefarijika ila nashida nimemtenda bwana dhambi nisio ijua namna ya kuiondoa inanites na naambiwa hua haisameheki naumia

  • Mpendwa,
   Usiogope, Mwambie Mungu naye atakusamhe, hakuna mtu anayeweza kukwambia lolote la kukukatisha tamaa, Mungu anaweza kukusamehe, kama wewe mwenyewe utaamua kutubu kweli na kuacha dhambi hiyo, tunajua kuwa sisi ni wanadamu tunaweza kurudi dhambini lakini Mungu wetu ni mwema na unapoamua kuanza upya hawezi kukuacha. kumbuka katika Isaya. 1:18 Mungu anasema
   “Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.”
   Mungu yupo tayari kukupokea ulivyo. Hukumu za Mungu ni tofauti na binadamu, mtu ataweza kukwambia huwezi kusamehewa na Mungu, lakini hilo si kweli, kumbuka mafarisayo walimleta kwa Yesu mwanamke aliyefumaniwa na wakataka kumpiga mawe lakini Yesu alipowaambi kama hakuna mwenye dhambi na aanze kutupa jiwe, dhamiri ziliwashitaki na wote wakaondoka, na ndipo “Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena”(Yohahe 8:10-11). Basi kama Yesu aliweza kumsamehe huyu mwanamke, bila shaka yeyote anaweza kukusamehe na wewe. lililo kuu ni wewe kuamnua moyoni mwako kuwa umejisamehe wewe na kuangalia mbele.

   Yote yanawezekana kwa Mungu. nakuombea kwa Mungu akupe msamaha wake na uwe na Amani.

   Sala ya Kuomba Msaada (https://nenolafaraja.wordpress.com/ee-mungu-uniokoe/)
   Sala ya Kuomba Msamaha (https://nenolafaraja.wordpress.com/ee-mungu-unirehemu/)
   Sala ya Baraka (https://nenolafaraja.wordpress.com/sala-ya-baraka/)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.