NITAFUNGAJE MWEZI HUU WA KWARESMA?

 • Acha kuongea maneno ya kuumiza, ongea wema kwa wengine
 • Acha huzuni , kuwa na moyo wa shukrani
 • Acha Hasira , kuwa mvumilivu
 • Acha tamaa, kuwa na matumanini
 • Usiwe mwoga , Mwamini Mungu
 • Acha kulalamika, kuwa na unyenyekevu
 • Acha kuwa na wasiwasi, kuwa mtu wa sala
 • Ondoa uchungu, jaza furaha moyoni mwako
 • Acha ubinafsi kuwa na huruma kwa wengine
 • Sahau ya zamani , samehe waliokukosea
 • Zungumza kidogo, Sikiliza Zaidi.

 Maneno ya papa Fransisko
Courtesy: tafsiri isiyo rasmi -whatsapp

Unazaa Matunda?

Mpendwa,

Je maisha yako ni kama mzabibu unaozaa matunda, je wewe ni mfano wa maisha ya Kimungu au wewe ni kikwazo, Mungu anatoa nafasi ili kujiweza safi kiroho, unajipangaje, usipozaa matunda, usipoishi maisha ambayo yanampendeza Mungu na wanadamu , basi utakatwa kama mzabibu usiozaa. “ Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate. Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu? Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate.”  Luka 13:7-9

Mungu tu, hufungua siri zote

Mpendwa,

Nakusalimu kwa jina la Bwana .

Siku zote katika maisha unapokuwa na jambo ambalo hujui suluhisho lake, mwendee Mungu naye atakufanya kujua suluhisho lake, yeye ndiye ajuaye siri ya kila fumbo hapa duniani, usimweleze mwanadamu siri zako, kwani mwanadamu si kitu na hawezi kufumbua siri za matatizo au maswala yanayotusibu.  Mkumbuke mfalme Nebukadreza, nsoto yake haikuweza kutafiriwa na watu, bali Daniel ambaye aliomba hekima ya mungu kujua ndoto na tafsiri yake. Ndipo Danielii akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake; ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo, ili kwamba Danielii na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli. Ndipo Danielii alipofunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku. Basi Danielii akamhimidi Mungu wa mbinguni.” Daniel 2:17-19,

Upendo

Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote

1 Kor 13:4-7