Sala Kabla ya Kulala

Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi. Wewe Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu ninayekutumaini.  Maana Wewe unaniokoa na mtego wa mwindaji na adui yangu, Na katika tauni iharibuyo. Kwa manyoya Yako unakufunika, Chini ya mbawa Zako nitapata kimbilio; Uaminifu Wako ni ngao na kigao. Sitaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana, Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri, Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pangu. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hawatanikaribia mimi kwa maana wewe unanilinda usiku huu. Kwa kuwa Wewe Bwana ndiwe kimbilio langu Mabaya hayatanipata katika usiku huu, Wala tauni haitaikaribia nyumba yangu, Kwa kuwa utaniagizia malaika zako Wanilinde usiku huu na siku zote katika njia zangu zote. Mungu Baba naweka usiku huu juu yako, Asante kwa kunilinda. Naomba na Kushukuru kwa njia ya Kristu Yesu Bwana wetu. Amina

Zaburi 19:1-10